LIVE STREAM ADS

Header Ads

MTUHUMIWA WA UJAMBAZI AUAWA NA POLISI JIJINI MWANZA WAKATI AKIJARIBU KUTOROKA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na BMG
Mtuhumiwa mmoja wa ujambazi na unyang'anyi wa kutumia silaha, ameuawa na polisi Jijini Mwanza, wakati akijaribu kutoroka huku watuhumiwa wengine wakitiwa mbaroni.

Taarifa iliyotolewa leo na Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, Naibu Kamishina wa Polisi, Ahmed Msangi, imeeleza kwamba tukio hilo lilitokea jana, wakati mtuhumiwa huyo alipowapeleka polisi katika eneo la Buhongwa Mlimani alikodai ameficha silaha.

Kamanda Msangi amesema mtuhumiwa huyo ambae alifahamika kwa jina la Msafiri Suleiman (Juma Msukuma), alikamatwa jana katika eneo la Igoma ambapo aliwapeleka askari katika eneo hilo la Buhongwa Mlimani alilokodai ameficha silaha na kuonyesha mkasi wa kukatia vyuma na kipande cha nondo huku akisema bunduki ameichimbia chini.

Ametanabaisha kwamba wakati polisi wakichimba eneo lililodaiwa kuwa na bunduki, mtuhumiwa huyo akiwa na pingu mikononi alianza kukimbia ambapo polisi walipiga risasi tatu za onyo angani lakini hakusimama ndipo polisi wakampiga risasi za miguuni na kutokana na majeraha ya risasi miguuni akakamatwa na wakati akipelekwa hospitalini akafariki dunia akiwa njia kutokana na majeraha ya risasi ambapo mwili wake umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa Bugando kwa ajili ya utambuzi.

Amesema awali mtuhumiwa huyo aliwataja wenzake aliokuwa akishirikiana nao katika uhalifu kuwa ni Jackson Magesa (Nyakibiriri), Samwel Mwita (Machage), Boniphace Nyamuhanga (Saroch) ambao tayari wametiwa mbaroni na polisi.

Amebainisha kwamba watuhumiwa hao walikuwa na silaha mbalimbali ikiwemo magazini moja ya bunduki aina ya Rifle Mark 4 ikiwa na risasi nne, nyundo moja, vipande vitatu vya nondo pamoja na kitako cha bunduki ambapo wanahusishwa na matukio ya uhakifu yaliyotokea katika maeneo ya Nyashishi, Buhongwa, Bulale, Nyambichi na Mwananchi Jijini Mwanza. 

Kamanda Msangi amewasihi wananchi kuwa watulivu huku wakiendelea kushirikiana na jeshi la polisi katika kutoa taarifa za uhalifu ili wahalifu wote waweze kukamtwa huku akiwaonya wale wenye mpango wa kujihusisha na uhalifu kuacha mara moja na kutafuta shughuli halali ya kufanya kwani jeshi la polisi halitawafumbia macho.

No comments:

Powered by Blogger.