LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI ATOA ONYO KALI KWA WATAKAOLETA VURUGU NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

"Kila mmoja afanye siasa kwenye eneo alilochaguliwa, Kingu mbunge wa ikungi magharibi afanye mikutano palepale kwake alipoahidi shughuli za maendeleo, Mbowe afanye siasa palepale hai alipochaguliwa na kuahidi kuwapa maendeleo,kila mmoja aliyechaguliwa afanye siasa eneo lake.

Sitaki kuona mtu anatoka HAI anakwenda KAHAMA kufanya mikutano n.k Mbunge au Diwani wa HAI au Mbeya anamamlaka ya kuingia kwenye vikao vya maendeleo ndani ya majimbo yao,huwezi kuwa Mbunge wa Ubungo vikao vya maendeleo ukafanyie Tarime.

Mimi (Rais) pekee ndiye natakiwa kuzunguka nchi nzima kila jimbo kufikisha maendeleo niliyowaahidi watanzania wote. Wanaotaka kuandamana au kufanya mikutano kiholela kwanini wanasubiri mwezi wa tisa?

Wafanye mikutano hata leo ili wajue mimi ni nani. Siwezi kugeuza hii nchi ya siasa, nataka nchi ya maendeleo tu. Siasa zilishakwisha wakati wa KAMPENI,muda huu ni KAZI TU". JPM.

No comments:

Powered by Blogger.