LIVE STREAM ADS

Header Ads

NAVY KENZO KUUNGANA NA WASANII WENGINE KUNOGESHA SHINDANO LA MISS TANGA 2016.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Tanga Raha
Wasanii wanaounda kundi la Muziki wa Bongo Fleva nchini Tanzania la Navy Kenzo, Nahreel na Aika, wanatarajiwa kutumbuiza kwenye shindano la kumtafuta malkia wa Mkoa wa Tanga, Miss Tanga 2016, litakalofanyika Julai 29 mwaka huu kwenye ukumbi wa Hotel ya Tanga Beach Resort.


Licha ya Navy Kenzo, wasanii wengine ambao watasindikiza onyesho hilo kwa kutoa burudani ni kundi la mziki wa kizazi kipya mkoani Tanga,Wazenji Classic pamoja na Dances.


Akizungumza jana, Mratibu wa Onyesho hilo, alisema kuwa maandalizi ya kuelekea shindano hilo yanaendelea vizuri ambapo tayari warembo watakaoshiriki wameanza kuingia kambini.


Shindano hilo ambalo limeandaliwa na kituo cha Radio cha TK FM 88.5 kilichopo mjini Tanga kwa kushirikiana na Hotel ya Tanga Beach Resort wameelezea namna walivyo jipanga kuhakikisha onyesho hilo linakuwa na ushindani mkubwa kutokana na aina ya warembo waliopo .


“Nisema tumejiandaa vizuri kuhakikisha shindano hilo linafanyika kwa umakini mkubwa ili kuwawezesha wadau wa tasnia ya urembo mkoani hapa kuweza kupata ladha halisi ya onyesho hilo kwani licha ya kuwaona warembo wakali wakini pia mzee wa kamatia chini atakuwepo kuwapagawisha “Alisema.

Hata hivyo alisema kuwa mazoezi ya warembo watanaoshiriki onyesho hilo yanaendelea kwenye ukumbi wa New Hotel uliopo mjini hapa kuanzia saa kumi jioni.


Aidha alisema kuwa kabla ya kufanyika shindano hilo warembo hao watapata fursa ya kutembelea maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii mkoani hapa ikiwemo Mapango ya Amboni na Hifadhi ya Taifa ya Saadani.

No comments:

Powered by Blogger.