LIVE STREAM ADS

Header Ads

DKT.KIGWANGALLA AHITIMISHA ZIARA YA KUWASHUKURU WANANCHI JIMBONI KWAKE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

DSC_2519
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla akiingia kucheza sambamba na vijana wa Sungusungu wa Jadi

Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla amemaliza ziara yake ya kuwashukuru Wanachi wa Jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao huku akiwaahidi kuendelea kushirikiana nao katika shughuli za kimaendeleo kama alivyotoa ahadi katika uchaguzi uliopita.

Katika ziara hiyo iliyoanza Julai 13 na kufikia tamati Julai 20, mwaka huu, Dk. Kigwangalla ameweza kuzunguka Vijiji mbalimbali vilivyo katika Kata 19 za Jimbo hilo ambapo amekutana na wananchi hao na kutoa shukrani zake.

Dk. Kigwangalla katika ziara hiyo, amewaomba Wananchi wa Jimbo hilo waendelee kumuombea kwani kazi ndio imeanza na kuwataka wananchi hao kushirikiana nae bega kwa bega katika shughuli za kimaendeleo.

“Kwanza nashukuru kwa kura zenu. Hakika zilitosha kuniwezesha mimi kuwa Mbunge. Kwa kura zenu nyingi pia zimewezesha kumpata Rais wetu Dk. Magufuli na Madiwani wengi katika Jimmbo hili. Nawashukuru sana Wana Nzega Vijijini” alieleza Dk. Kigwangalla.

Aidha, Dk. Kigwangalla katika ziara hiyo, alipata wasaha wa kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo sehemu za shule, Vituo vya Afya ambapo alijioenea hali ilivyo huku akieleza kuwa ataendelea kushirikiana na Watendaji wote wa ngazi ya Kijiji, Kata na ngazi za juu.

Dk. Kigwangalla pia aliweza kutoa misaada ya vifaa vya michezo kwa vijana mbalimbali ambapo awali aliwaahidi yeye mwenyewe.
Kata zinazounda Jimbo hilo la Nzega Vijijini ni pamoja na Kata ya Puge, Ndala, Nata,, Sanzu, Lusu, Milambo Itobo, Magengati, Budushi, Nkiniziwa, Mbagwa, Mizibaziba, Utwigu, Muhugi, Mwantundu, Wela, Mwasala, Tongi, Ugembe na Mwakanshanhala.
Aidha, Dk.Kigwangalla alipata wasaha wa kushiriki mazishi ya Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdalla Simba ambaye alikuwa mwenyekiti wa CCM Kata wa Nzega Magharibi aliyefariki Julai 19 jioni.

Marehemu Mzee Simba ambaye alikuwa mkongwe kwenye chama hicho tokea chama cha TANU ambapo aliwelezewa kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kukiunganisha chama cha TANU na baadae CCM.

Mpaka umahuti unamkuta alikuwa Mwenyekiti wa CCM wa tawi hilo. Dk. Kigwangalla pia alipata kutoa ubani na kuwajulia pole ndugu wa wafiwa.

No comments:

Powered by Blogger.