LIVE STREAM ADS

Header Ads

WATUMISHI WA HALMASHAURI MPYA YA USHETU MKOANI SHINYANGA WATAKIWA KUHAMIA MAKAO MAKUU YA HALMASHAURI HIYO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Shaban Njia
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinya, Fadhili Nkulu, ametoa muda wa siku moja kwa Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, kuhakikisha kuwa wanahamia katika Makao Makuu ya Halmashauri  hiyo yaliopo Nyamilangano.

Nkulu aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na Waandishi wa Habari ofisni kwake, muda mfupi baada ya kikao na Watumishi hao katika Makao Makuu ya Halmashauri hiyo yaliyopo katika kata ya Nyamilangano Halmashauri ya Ushetu.

Alisema kuwa kitendo cha Watumishi wa Halmashauri ya Ushetu iliyopo Wilayani Kahama, kuhamia katika kata hiyo kitaharakisha maendeleo katika Halmashauri hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.