LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI AWAFURAHISHA WAKAZI WA MKOANI GEITA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Rais Dkt.John Pombe Magufuli ametoa muda wa wiki tatu kwa mamlaka mkoani Geita, kuandaa utaratibu mzuri ili wananchi waanze kupewa mawe yenye mabaki ya dhahabu (magwangala) ambayo yamerundikana katika baadhi ya migodi mkoani humo ikiwemo GGM.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jioni hii, wakati akiwahutubia wananchi wa mkoani humo, kwenye mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wananchi kwa kumchagua uliofanyika katika uwanja wa CCM Kalangalala huku wananchi wakimshangiliwa kila alipokuwa akizungumzia suala la magwangala.

Rais Magufuli amesema haiwezekani wananchi kuzuiliwa kuchukua magwangala hayo na wawekezaji kwani magwangala hayo ni mali ya wananchi maskini.

Ametoa muda wa wiki tatu kwa Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC, kushirikiana na viongozi mkoani Geita kuanza kugawa magwangala hayo huku akiwasihi wananchi kuwa watulivu katika zoezi hilo kwani wakiyagombania na kusababisha madhara ikiwemo vifo, atasitisha zoezi hilo mara moja. Amesema utaratibu wa kugawa magwangala hayo kwa wanachi utakuwa endelevu badala ya kuyaacha yanarundikana tu.

Aidha amewataka viongozi wa bodi ya pamba kuhakikisha kwamba wanahamia katika mikoa inayolima zao la pamba ambayo ni pamoja na Geita, Mwanza, Mara na Shinyanga, badala ya kukaa Jijini Dar es salaam ambako zao hilo halilimwi huku akionya juu ya suala la bodi hiyo kusambaza kwa wakulima mbegu ambapo amesema yeyote atakayegawa mbegu za pamba na zisiote ajiandae kuondoka.

Rais Magufuli ambae amewasili mkoani Geita akitokea mkoani Shinyanga, amesisitiza kwamba muda wa siasa umekwisha na ataendelea kuwa mkali kwa ajili ya maendeleo ya Tanzania na kila kiongozi lazima aendane na kasi yake na kuwataka wananchi wafanye kazi kwa bidi.

No comments:

Powered by Blogger.