LIVE STREAM ADS

Header Ads

SOMA UCHAMBUZI MAALUMU KUHUSU SERA YA MAENDELEO YA VIJANA NCHINI TANZANIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Edwin Soko ambae ni Mchambuzi na Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uharifu. Pia ni Mratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mwanza. (Picha Kutoka Maktaba-BMG)
1:Nini  Maana  ya Sera?
Ni  mpango, hunaoweza  kuandaliwa  na serikali, chama cha  siasa au biashara ikiwa inalenga  kutoa ushawishi utakaopelekea kufanywa  kwa  maamuzi , vitendo na hatimaye  kupata  mafanikio.
Sera   ta  Taifa  ta  Maendeleo  ya  Vijana  inatoa  mwongozo  si  tu kwa  vijana, wazazi  na waelimishaji bali  kwa  jamii  nzima  na hasa  kwa  wapangaji  wa mipango  ya   maendeleo   katika  sekta  mbalimbali za maendeleo.

2:Maana  ya kijana
Inaweza  kutofautiana  kutokana  na mila, desturi na tofauti za maadili  katika jamii  mbalimbali  na mahali walipo. Kijana ni  mvulana  au mwanamke  ambaye  yupo  katika  rika la utoto  kuelekea  rika la utu uzima.  Kuligana na  tofauti  mbalimbali   sera  hii  imetumia  fafsiri  ya  kijana  kutokana na tamko la  Umoja wa Mataifa ambapo kijana  ni mtu  mwenye  umri kati  ya  miaka  14- 24.

3:Historia  hadi  kutungwa kwa Sera
Tangu  Tanzania  ipate  uhuru  wake  mnamo   mwaka 1961  hapakuwa na  Sera  rasmi  iliyoandaliwa   kwa  ajili    ya  malezi  na maendeleo  ya  Vijana . Masuala  ya  malezi na maendeleo  ya  vijana  kwa kipindi  chote hicho  yalikuwa  yakitekelezwa  kupitia  Sera  nyingine katika mipango  ya  maendeleo, kampeni, maazimio  na miongozo ya  chama tawala  na  Serikali.

Sera hii iliandaliwa kwa ajili ya kusimamia maslahi ya kijana, ambayo serikali iliandaa mwaka 1996 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007,  Sera ya taifa ya maendeleo ya vijana ya 2007 inalenga masuala ya maendeleo ya vijana ambayo ni pamoja na: uwezeshaji wa kiuchumi, mazingira, VVU na Ukimwi, jinsia, sanaa na utamaduni, michezo afya ya uzazi kwa vijana na masuala ya maisha ya familia.

4:Msingi wa Sera
Msingi wa  sera  unatokana na uzingatiaji wa haki za binadamu kama zilivyotajwa  katika  katiba  ya  Jamhuri  ya  Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977  na kufanyiwa  marekebisho  mwaka 1984 na 1995.  Haki  hizi ni  pamoja  na haki  ya  kuishi, kulindwa, kuendelezwa  na kujiendeleza, kushirikishwa  katika  shughuli za maendeleo  yake  na  jamii. Haki  nyingine  kulingana  na  katiba hiyo ni pamoja  na  haki  ya kutobadiliwa , kuheshimiwa, kumiliki mali na rasilimali, kufanya  kazi  na  kupokea  matunda  ya  kazi  hiyo pamoja na mbele  ya sheria  za Nchi.

4:Lengo  la  Sera
  • Kuhakikisha Taifa linakuwa na vijana wenye uwezo, wenye ari ya kutosha , wawajibikaji na wanaoshiriki kikamilifu katika Nyanja zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi kwa maendeleo ya jamii.
  • Kuweka mazingira yanayowezesha kujenga uwezo wa vijana na kukuza nafasi za ajira na kupata huduma ya hifadhi ya jamii
5:Uchambuzi
Sera  ina  sehemu    kuu  Tano (5)
5:1 Sehemu ya kwanza:
Hii  inaeleza  utangulizi    kwa mujibu wa  miongozo  ya  kisera
5:2 Sehemu ya pili:
·         Umuhimu wa sera
·         Dhamira
·         Dhima
·         Malengo

5:3 Sehemu  ya  Tatu
Sehemu hii  imebeba  mambo (29)  yakiwemo:
  • Mambo  kisera  na maelezo  yake
  • Tafsiri sahihi ya   kijana
  • Mzingira  ya  vija  kuishi  kwenye  dimbwi la matatizo
  • Maandalizi  ya  kijana  ili aishi kwa kufuata  misingi  ya  jamii
  • Rasilimali  zinazoweza kumwinua kijana  na  kumwendeleza
  • Huduma  za kifedha  zninazoweza kuondoa  umaskini kwa kijana
  • Ushiriki wa vijana  kwenye  kilimo  na  ufugaji
  • Nafasi za vijana  kwenye  serikali za mitaa   na uongozi wa Mkoa
  • Haki za kijana
  • Misingi ya usawa wa  kijinsia kwenye  maendeleo
  • Mifumo  ya kisheria  ya  kumwendeleza kijana
  • Vijana na sekta  ambazo  si  rasmi
  • Chombo  cha  kisheria  cha kuwaunganisha  vijana
  • Ushiriki wa kijana  kwenye  kumwelndeleza  kijana
  • Kijana  na  fursa  za  ajira
  • Vijana na madhira  ya  Ukimwi
  • Matumizi ya  TEHAMA  Kwa  vijana
  • Kijana  na ulemavu
5:4 Sehemu ya Nne
-Majukumu  ya wadau
  • Wazazi na  walezi
  • Mashirika ya dini, taasisi zisizo  za kiserikali, sekta  binafasi  na asasi za kijamii
  • Serikali za Mitaa  na  uongozi wa Mkoa
  • Serikali kuu
  • Wadau wa maenedeleo
5:5 Sehemu ya  Tano:
-Mpangilio wa utekelezaji
-Hupatikanaji wa huduma za kijamii
-Usimamizi wa  program, ufutiliaji  na  tathimin

6:0 Mtazamo
Kimsingi  Suala  la   Taifa  kuwa  na  sera  ya  Vijana   limechelewa  kwa  kiasi  kikubwa  kwani tumepata  sera  hiyo    mwaka 2007  wakati wenzetu  Kenya  ilikuwa  na sera  hiyo  mwaka …………….  Uganda  mwaka ……………..

Mwanasisasa  Zitto  Kabwe  hakukosea  kusema  kuwa  Taifa  hili ni  Taifa  la  Vijana na watoto, kwani  kwa mujibu  wa  sensa  ya  watu  na  makazi    Vijana  wamebeba  asilimia  33/%   ya  watu  wote.

Vijana  na  Uchumi wa Nchi

Nchini   Tanzania  vijana    wengi  wamekuwa  wakijihusisha  katika  sekta  za kilimo, uvuvi, madini, ufugaji  na uwekezaji  kwenye  viwanda  vidogovidogo  kama    utengenezaji wa  matunda, vitua  asilia na  vinginevyo.

UCHAMBUZI
Kwa kiasi  kikubwa  sera   imeakisi  matatizo  ya  vijana   wa kitanzania  na  pia  kutoa  mwelekeo  mzuri  sana  wa kuyashughulia  matatizo  hayo.
Mfano:

Suala  la  ajira  kwa  vijana
Kama  tujuavyo  kuna  vijana  wengi  wanaomaliza  elimu  ya msingi, sekondari  na  vyuo  vya  juu  wakikosa  ajira   na kuangukia kwenye  sekta  zisizo  rasmi, ambazo  huko  hakuna   job  security, kukosekana kwa mitaji  

Kauli  ya  sera
  • Serikali  kwa  kushirikiana  na  sekta  binafsi  itaandaa  mazingira  mazuri  ya  kutengeneza  ajira  kwa  vijana.
  • Kuwa  na sera  ya  Taifa  ya  ajira
  • Kuwa  na sera  ya  undelezaji  maeneno  ya vijijini na kilimo (Rural Development Strategy and Agricultural Development Policy.
  • Serikali  kushirikiana  na  taasisi  binafsi   na wadau  wengine  kutoa  elimu ya  ujasiriamali  kwa  vijana  ili waweze kujiajiri.
Ushirikishwaji wa  vijana  na  Utawala  Bora
Vijana    wanamchango  wa 65%    ya  nguvu kazi  ya  wazalishaji wa  uchumi wa  Taifa (Labour  Force)  lakini    35%    ya  vijana  hao  hawawakilishwi  vyema kwenye  forums  mbalimbali za ngazi  ya  maamuzi, na matokeo  yake  maamuzi  mengi yanayofikiwa  hayagusi  matatizo  ya  vijana.

Kauli  ya sera
Mifumo   ya  halamashauri za    serikali za mitaa  na  serikali  kuu  iwe  na mifumo  inayotambua  uwepo wa jina  na  pia  uwakilishi  kwenye  ngazi  nyingine  za kitaifa  na kimataifa

Kuwa  na  chombo cha  kuwaunganisha  vijana
Kwa muda  mrefu  kulikuwa    hakuna  chombo  chenye  nguvu  kinachoweza kuwaleta  vijana  pamoja na kutambua  matatizo   yao.

Kauli  ya  sera 
Kuundwa  kwa  chombo kitakachoweza kuwasemea  vijana “ Uuundwaji  wa  Baraza  la Vijana Taifa”

Huduma  za kifedha  na mkakati wa  kupunguza  umaskini
Kuna  mikakati mingi  iliyopitishwa  kwenye  kuwainua  vijana kwa kuwapa misaada   ya  kifedha ili waweze  kujiinua  kiuchumi, lakini  mikakati hiyo  imekuwa  si  endelevu, wala  mpangilio  mzuri

Kauli ya    sera
  • Kuwa  na mkakati  endelevu  wa  kuwasaidia  vijana kifedha  ili waweze kujiinua  kiuchumi
  • Kusisitiza  umuhimu wa kuwa na mfuko wa  wa  fedha  wa kuwasaidia  vijana.
Nafasi  ya  vijana  kwenye  muundo wa  Serikali za mitaa
Muundo wa  Serikali  za mitaa   hakuweza  kuwa  na uwakilishi  mzuri  wa  kutambuamatatizo  ya vijana, kwa kuwa  hakukuwa  na Afisa    anayeshughulikia   uendelezi  wa kada  ya   vijana, hii  ilifanya  kuwa  na mfumo  dhaifu  toka  serikali  kuu  hadi  serikali  za mitaa.

Kauli ya  Sera:
  • Kuwe  na up -  down   approach   wa kutoa  uwakilishi  toka   ngazi za  kata  hadi  Taifa, hilo  liwe  jukumu  la  wizara    husika  ya serikali za mitaa na  serikali  kuu
  • Serikali  kuu  na serikali za mitaa iweke  utaratibu  wa kuajiri  Afisa  atakayehusika  na undelezaji wa kada  ya  vijana
Vijana  kuishi  kwenye  mazingira  magumu
Kuna  vijana  wapatao  million  2  yatima  wanaoishi kwenye  mazingira  magumu sana  ya kimaisha

Kauli  ya sera
Sera  imeelekeza kuwa, kuna  mkakati  wa kuwawezesha  kupata  fursa  kwenye  elimu, mafunzo na usalama  wao kwa wote  waliokubwa na  matatizo  hayo.

Maandalizi  kwa kijana  ili  awe  raia  mwema  kwenye  jamii
Vijana  wametakiwa  kuwa   na  maandalizi  mazuri  ili waweze  kutimiza  wajibu wao  kwenye  jamii wa kuwa  raia  wema.

Kauli ya  sera
Kuwa  na  mkakati  maalumu  wa kuandaa  miongozo  ya  malezi  kwa  vijana

Matumizi  ya  rasimimali za Nchi  zinazoweza kuwainua  vijana
Tunaelewa  wote  kuwa  Nchi  yetu ina rasilimali nyingi, ambazo  zikitumika  vizuri  zinaweza  kuwasaidia sana  vijana  kuinua  maisha  yao.  Rasilimali  hizo  ni  kama  ardhi na nyinginezo
Kauli  ya  sera .   Kwa mujibu wa      integrated   labour   survey 2001,  asilimia  65  ya  wazalishaji  wa  uchumi  wa Nchi ni  Vijana.

Kauli  ya  sera
Kutakuwa  na  kipaumbele  cha  rasimimali za  Nchi  kwa kundi la  vijana

Matumizi ya    TEHAMA
Vijana wengi  wamekuwa  wakitumia  teknolojia  kwa  mtazamo   hasi  badala  ya  chanya, kama kutumia  kwa  kukuza weledi wa kitaaluma    wao  wanatumia kwa    kutazama  vitu  vinavyoweza  kumomonyoa  maadili ya  Taifa

Kauli ya  sera
Kuwa  na  makakati wa  kufuatilia  maudhui  ya  matumizi  ya  teknolojia

Mapungufu/Gap
Sera  yetu    ina  mapungufu machache  kama  kutoweka   kipaumbele  kwa makundi  maalumu,  hii  inasababisha  baadhi  ya  makundi  Kutopewa kipaumbele,  Sera  ya  maendeleo  ya  vijana  ya  Kenya  yenyewe  imeweka vipaumbele  kwa  makundi  maalumu  ya vijana  kama walemavu, waathirika  wa HIV, wanawake, vijana  wasio na ajira  na  wale waliokosa  fursa za kusoma.

HITIMISHO
Sera  ya  Maendeleo  ya  vijana  ni  nzuri  kwani  imeanisha  matatizo  ya  vijana  na kutoa  njia  sahihi  ya  kuyashughulikia,  tatizo  kubwa   linalojitokeza  hapa  ni  kama  matatizo  ya  sera  nyingine  za Nchi hii suala  zima  la  utekelezaji  wa sera (Implementation) tu.

Endapo  Serikali  ya  awamu  ya  tano  itaamua  sasa  kuisimamia  sera  hii  kwa kuitekeleza  ni wazi  kuwa   kijana    kada  ya  vijana    itaboreka na kutoa  mchango  mkubwa  kwenye     falasa  ya  seriklai  ya  John  Pombe   Magufuli  ya  kwenda kwenye  uchumi wa  kati wa  Viwanda.

Naomba  kuwakilisha
Edwin Soko
PhD  Candidate  

Kumbuka Soko amewasilisha Uchambuzi huu hii leo katika Kongamano la Vijana Wajasiriamali na Wawekezaji mkoani Mwanza. TAZAMA HAPA.

No comments:

Powered by Blogger.