LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA MSD JUU YA UAMUZI WA BODI YA WADHAMINI KUHUSU WAKURUGENZI WALIOSIMAMISHWA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
BMG tumenakiri taarifa hii ili uisome vyema.
Taarifa kwa Umma, Uamuzi wa Bodi ya Wadhamini Kuhusu Wakurugenzi waliosimamishwa.

Mnamo tarehe 15/2/2016 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy A. Mwalimu (Mb) alitoa maelekezo kwa Bodi ya Wadhamini ya Bohari ya Dawa (MSD) kuwasimamisha kazi Wakurugenzi wanne (4) wa Taasisi hiyo ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinawakabili.

Wakurugenzi hao ni pamoja na Mkurugenzi a Shughuli za Kanda na Huduma kwa Wateja Bw.Cosmas Mwaifwani, Mkurugenzi wa Fedha na Mipango, Bw.Joseph Tesha, Mkurugenzi wa Ugavi, Bw.Misanga Muja na Mkurugenzi wa Ununuzi Bw.Heri Mchungu, Uchunguzi juu ya Wakurugenzi hao umekamilika.

Katika kikao chake kilichofanyika tarehe 8/7/2016, Bodi ya Wadhamini ya MSD iliamua yafuatayo:

i. Bw.Heri Mchunga ameonekana hana makosa, hivyo anarudi kazini kuanzia tarehe 12/7/2016. Hata hivyo Bwana Mchunga amehamishiwa Kurugenzi ya Ugavi kuwa Mkurugenzi.

ii. Bw.Joseph Tesha anarejeshwa kazini kuanzia tarehe 12/7/2016 lakini uteuzi wake wa nafasi ya Ukurugenzi umetenguliwa, hivyo atapangiwa kazi nyingine.

iii. Bw.Misanga Muja aliyekuwa Mkurugenzi wa Ugavi anarejeshwa kazini kuanzia tarehe 12/7/2016, lakini uteuzi wake wa nafasi ya Ukurugenzi umetenguliwa na atapangiwa kazi nyingine.

iv. Bw.Cosmas Mwaifwani amepatikana na makosa, na ameachishwa kazi kuanzia tarehe 8/7/2016.

Maamuzi ya Bodi ya Wadhamini yamezingatia Kifungu cha 12(a) cha Sheria ya Bohari ya Dawa Na.13 ya mwaka 1993 ikisomwa pamoja na Kanuni ya 7 na ya 73(2) za Utumishi wa MSD, 2015.

Imetolewa na:
Laurean Rugambwa Bwanakunu
KATIBU WA BODI YA WADHAMINI NA MKURUGENZI MKUU

No comments:

Powered by Blogger.