LIVE STREAM ADS

Header Ads

UMOJA WA KIJAMII CHUO KIKUU STEFANO MOSHI WATEMBELEA KITUO CHA KUELELEA WATOTO KILIMANJARO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Baadhi ya watoto wanaoishi na kulelewa katika kituo cha Kilimanjaro Orphanage Centre
Wanaumoja wakiwa katika picha ya pamoja katika lango kuu la kuingia chuoni hapo kwa kampasi ya mjini kabla ya kuelekea kituoni

Umoja wa Kijamii (UKI) ulioanzishwa na wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University wenye lengo la kuitumikia jamii kwa kujitolea kupunguza changamoto za ukali wa maisha katika jamii ulipata fursa ya kukitembelea kituo cha kulea watoto yatima na wenye mahitaji maalum cha Kilimanjaro Orphanage Centre kilichopo kata ya Pasua wilaya ya Moshi mjini  mkoa wa Kilimanjaro.

Akizungumzia historia yao, Mkurugenzi wa kituo hicho Bw. Lazaro Edward alisema kituo hicho kinachopokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu na kuendelea kwasasa kinalea  watoto wapatao 79 huku watano kati yao wakiwa ni waathirika wa virusi vya Ukimwi  kueleza kuwa changamoto kubwa inayowakabili ni idadi ya vitanda pamoja  udogo wa eneo lakini wanatarajia kukihamisha kituo hicho baada ya ujenzi wa kituo rasmi kukamilika.

Akizungumzia ziara hiyo mmoja kati ya wanaumoja huo, Godilisten Mnuo, alisema kuwa amejifunza mambo mengi hasa upendo kutoka kwa watoto hao na kutoa wito kwa wadau mbali mbali kuwa na tamaduni ya kudumisha uhusiano na wenye mahitaji kwa moyo wa dhati katika jamii ili kwani hii ndio sifa bora machoni pa Mungu na wanadamu.
Wana UKI wakikaribishwa na kupewa maelezo ya awali kutoka kwa Mkurugenzi wa kituo hicho Bw.Lazaro Edward mara tu walipowasili 
Wana UKI wakicheza na watoto wa Kilimanjaro Orphanage Centre
Watoto wakiteta jambo huku nyuso zao zikiwa na tabasamu la kutembelewa na wageni
Kulia ni mwenyeketi wa UKI Bw. Msiyaki Kuruchumila akikabidhi zawadi kwa watoto hao
Mwenyekiti wa vijana CCM mkoa wa Kilimanjaro Juma Raibu (Kushoto) akiwa na Rais wa Serikali ya wanafunzi SMMUCo Edgar Nziku ambao wote  ni wana UKI wakiwa na watoto kituoni hapo
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA 


No comments:

Powered by Blogger.