BANDA LA CHUO KIKUU MZUMBE LAWAVUTIA WENGI KWENYE MAONESHO YA NANENANE KANDA YA ZIWA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Wananchi mkoani Mwanza pamoja na waliotoka mikoa mingine ya Kanda ya Ziwa, wamevutiwa na banda la Chuo Kikuu Mzumbe kwenye Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yaliyofanyika katika Uwanja wa Nyamuhongolo Jijini Mwanza kuanzia Agost Mosi hadi Agost 08,mwaka huu.
Wengi wao walifika katika banda hilo ili kupata elimu ya masuala mbalimbali ya kielimu ikiwemo mitaala inayofundishwa na chuo hicho sanjari na ratiba na sifa za wanaohitaji kujiunga na mhura mpya wa masomo ikizingatiwa kwamba usaili umeanza katika matawi mbalimbali ya chuo hicho nchini.
Pia wananchi walipewa vipeperushi mbalimbali vyenye maelezo muhimu kuhusiana na Chuo cha Mzumbe ambacho tawi lake kuu liko mkoani Morogoro huku kukiwa na matawi katika mikoa mingine kama Mwanza, Mbeya na Dar es salaam.
Na BMG
Wananchi wakisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Chuo Kikuu Mzumbe
Timu ya Chuo Kikuu Mzumbe ikitoa ufafanuzi kwa wananchi
Timu ya Chuo Kikuu Mzumbe ambapo kutoka kushoto ni Ally Maringo, Jaspar Mmbaga, Nsikwa Chisalala na Dkt.Fred Alfred.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.
No comments: