MADALALI WALALAMIKIWA KUKWAMISHA KAULI YA KASSIMU MAJALIWA JUU YA LUMBESA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Bwana Raphael Nkiru , Halphan Said, Rehema Muddy na Dionis Mafuru, wote wafanyabiashara kwenye Soko la Kirumba waliwalalamikia madalali wa Sokoni hapo kuwa, wanakwamisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa katazo la lumbesa.
“Kimsingi baadhi ya madalali wamekuwa wakitumwa na wafanyabiashara wakubwa toka Nchi za Kongo na Burundi kuwanunulia dagaa visiwani na huko wanatumia vipimo visivyo rasmi kwenye kununua dagaa na kuwaibia wakulima licha ya katazo la Serikali” walihitimisha wafanyabiashara hao.
Bwana Ben John dalali sokoni hapo alisema kuwa, wapo baadhi yao ambao wamekuwa sio waaminifu hasa wanapoenda kununua dagaa visiwani, ila yeye anazingatia maagizo ya serikali hawezi nunua dagaa kwa mfumo wa lumbesa pia kama wanakuja wateja wanaotaka kununua dagaa kwa mfumo wa lumbesa huwa anawafukuza.
Naye dalali ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa, suala la wao kununua dagaa kwa mfumo wa lumbesa halina ushahidi wa kutosha linahitaji muda mrefu ili kupata majibu sahihi.
Uchunguzi uliofanywa na makala hii uligundua uwepo wa Madalali wengi Sokoni hapo ambao wamekuwa wakijihusisha kuendesha biashara ya dagaa Soko la Kirumba kwa kuwa kiungo kati ya wafanyabiashara wakubwa na wauzaji wa dagaa, hali hiyo imekuwa kero kwa wauzaji wa dagaa kwani wanaona kuwa, wanaibiwa kupitia Madalali hao ili kuwanufaisha wafanyabiashara.
Makala hii imefadhiliwa na Mfuko wa Wakfu wa Tasnia ya Habari Tanzania (TMF).
Mwandishi, Neema Joseph (kushoto) akifanya mahojiano.
Na Neema Joseph, Mwanza
Baadhi ya wauzaji wa dagaa kwenye Soko la Kirumba Jijini Mwanza wamewalalamikia madalali Sokoni hapo kukwamisha vita dhidi ya lumbesa kama ilivyotolewa kwenye tamko la Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye katazo la lumbesa.Bwana Raphael Nkiru , Halphan Said, Rehema Muddy na Dionis Mafuru, wote wafanyabiashara kwenye Soko la Kirumba waliwalalamikia madalali wa Sokoni hapo kuwa, wanakwamisha utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa katazo la lumbesa.

No comments: