LIVE STREAM ADS

Header Ads

BINTI MWENYE ULEMAVU WA NGOZI WILAYANI TARIME AILILIA SERIKALI KUMSAIDIA MATIBABU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Cleo Newz
Binti mmoja Mkazi wa kijiji cha Kemakorere Kata Nyarero Wilani Tarime Mkoani mara Mwenye umri wa miaka 16 Maria Mahiya amezidi kuiomba Serikali kwa kushirikiana na mshirika mbalimbali ikiwemo jamii inayozunguka watu wenye ulemavu wa Ngozi albino kutoa msaada ili kuweza kutibiwa saratani ya sikio ambayo imedumu kwa muda mrefu bila kupona jambo ambalo linamusababishia maumivu makali.

Maria alisema kuwa alianza kupata upele katika sikio hilo ambapo baba yake mzazi alifanya jitiahada za kumpeleka Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Wilaya hadi mkoa lakini kadili alivyozidi kupata matibabu hali yake ilizidi kubadilika na kulazimika kupelekwa Hospitali ya Ocean Road lakini bado hali yake ni mbayo hivyo ameiomba serikali kumpa msaada ili kupata matibabu kwa lengo la kuokoa maisha yake.

“Mimi kwa kweli hali yangu ni mbaya sana naomba rais wetu akasikie kilio change na kunipeleka Nje ya Nchi ili nipate matibabu kwa ajili ya kunusuru maisha yangu jamani” alisema Maria huku akilia kwa uchungu.

Mahiya Matiko 43 ni baba mzazi mwenye watoto11 huku watoto wawili wakiwa ni walemavu wa Ngozi albino ambapo mke wake kwa sasa ni mwaka wa pili amefariki dunia hivyo family yake inamutegemea amesema kuwa kwa sasa ameisha uza malizake zaidi ya millioni moja ili kutibu mtoto wake ambaye anasumbuliwa na saratani ya sikio yenye uvimbe sikioni hivyo amezidi kutoa kilio kwa serikali na mashirika ili kumusaidia mtoto huyo.

“Jamani huyo mdogo wake alinusurika hivi karibuni kuibiwa na watu wasiojulikana sasanikampeleka kituo cha kutunza watoto wenye ualbinodada yake amekaa Dar es salaam takribani miezi saba ocean road hajapona amerudi kila siku ni lazima kuosha kidodo sina hata mia sasa mimi bora mungu amuchukue sina jinsi serikali inisaidi sasana watu wenye huruma kupitia namba0766128337” alisema Mahiya.

Eliza James ni katibu wa Chama cha watu wenye ualbino wilayani Tarime Mkoani Mara (TAS) watu wenye ulabino wamesahulika huku jamii imekuwa ikiwatenga na kusema kuwa adui wao mkubwa ni jua sasa serikali haina budi kuwasaidia ili waweze kujikwamua kiuchumi.


Sisi mbali na mauaji lakini hayo serikali imekomalia lakini adui wetu ni jua na wengi wenzetu hawajaenda shuleni na hatuwezi kufanya kazi za juani serikali isikie kilio chetu hususuani cha marai mwenzetu anaumia sana nimekwenda mwanza kumpokea akitoka kwenye ,matibabu hadi kufika Tarime nimembeba anamaumivu makali alisema Eliza.

No comments:

Powered by Blogger.