LIVE STREAM ADS

Header Ads

CHUO KIKUU CHA MZUMBE CHASHIRIKI MAONESHO YA NANENANE JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Chuo Kikuu Mzumbe ni miongoni mwa tasisi za elimu ambazo zimeshiriki Maonesho ya Wakulima na Wafugaji Nanenane yanayofanyika kwa Kanda ya Ziwa kwenye Uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Maonesho hayo ambayo yalianza tangu Agost Mosi mwaka huu, kwa Kanda ya Ziwa yalifunguliwa rasmi jana na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Ukifika katika Maonesho hayo, hakikisha unaenda banda la Chuo Kikuu Mzumbe ambapo utapata maelezo sahihi juu ya mihula na masomo yanayotolewa na chuo hicho kwa ngazi zote ikiwemo Cheti, Stashahada, Shahada na Shahada ya Uzamili.

Tawi kubwa la Chuo Kikuu Mzumbe liko mkoani Morogoro huku pia kukiwa na matawi katika mikoa mingine kama vile Dar es salaam, Mbeya na Mwanza.
Na BMG
Banda la Chuo Kikuu Mzumbe

Kulia ni Nsikwa Chisalala ambae ni Afisa Mdahili Mkuu, Chuo Kikuu Mzumbe akifafanua jambo kwenye banda la chuo hicho katika maonesho ya Nanenane Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Katikati ni Nsikwa Chisalala ambae ni Afisa Mdahili Mkuu, Chuo Kikuu Mzumbe akifafanua jambo kwenye banda la chuo hicho katika maonesho ya Nanenane Nyamhongolo Jijini Mwanza. Kulia ni Jaspar Mmbaga ambae ni Mratibu, Kituo cha Mwanza, chuo kikuu cha Mzumbe.
Kulia ni Nsikwa Chisalala ambae ni Afisa Mdahili Mkuu, Chuo Kikuu Mzumbe akifafanua jambo kwenye banda la chuo hicho katika maonesho ya Nanenane Nyamhongolo Jijini Mwanza.
Kushoto ni Ally Maringo, kutoka Chuo Kikuu Mzumbe akifafanua jambo kwenye banda la chuo hicho katika maonesho ya Nanenane Nyamhongolo Jijini Mwanza.

Tembelea www.sob.mzumbe.ac.tz au www.mzumbe.ac.tz kwa taarifa zaidi kuhusu Chuo Kikuu Mzumbe.
Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.