LIVE STREAM ADS

Header Ads

IDADI YA MAUZO SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM YAPANDA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
DSE Weekly Market Activity
Na James Slvatory
Idadi ya mauzo katika  Soko la hisa Dar es saaam (DSE) imepanda kwa asilimia 57% na kufikia TZS 3.3 Bilioni kutoka TZS 2.1 Bilioni huku Idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa zimepanda kwa 34%  hadi Milioni 2.2 kutoka Milioni 1.6

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam meneja mwandamizi wa soko la hilo Meryy Kinabo  amesema Kampuni tatu zinazoongoza kwa idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa ni  CRDB kwa asilimia 49%,DSE kwa asilimia 43%  na TBLkwa asilimia 4% huku Ukubwa wa mtaji wa soko umepanda kwa 0.67% na kufika Trilioni 23.4 kutoka Trillioni 23.2.Ukubwa wa mtaji wa makampuni ya ndani umebaki kwenye kiwango kile kile cha panda 8.4 Trillion

Aidha kinabo amesema kuwa Sekta ya viwanda (IA) wiki hii imeshuka kwa pointi19.47 baada ya bei za hisa za TBL kushuka kwa 0.66%. Sekta ya huduma za kibenki na kifedha (BI) wiki hii imepanda kwa pointi 29.89 baada ya bei kupanda kwenye kaunta za DSE kwa 10.67% na NMB 1.48% Sekta ya huduma za kibiashara (CS) wiki hii iko vilvile baada ya bei za hisa za Swissport kubaki TZS 3,543.02

Kwa Upande wa Shindano la Wanafunzi wa Vyuo Vikuu (DSE Scholar Investment Challenge 2016 mshindi wa kwanza ni Godfrey pantaleo makweka kutoka chuo cha institute of Accountancy Arusha na wa pili ni Benson Humphrey chuo cha sokoine universitynof Agriculture  na wa tatu ni frank kigodi kutoka university of Dodoma

No comments:

Powered by Blogger.