LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAULI YA KASSIMU MAJALIWA NI CHANGAMOTO KWA LUMBESA YA DAGAA MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na: Neema  Joseph, Mwanza
Kauli  aliyoitoa  Waziri Mkuu   Kassimu Majaliwa  mwanzoni  mwa  mwaka  huu  juu yakatazo   la   lumbesa   imekutana   na    changamoto    kubwa   kwa   upande   wa biashara   ya dagaa Jijini Mwanza,      kwani   sheria   ya vipimo  sura namba 340 ya mwaka 1982  imeshindwa  kuainisha  ujazo  rasmi wa  kutumika.

Meneja   wa   Wakala   wa   Vipimo   Mkoa   wa   Mwanza   Hemed   Kipengele   amekiri uwepo  wa mapungufu kwenye  sheria  hiyo, kwani licha  ya  sheria  kuanisha  vipimokwa   mazao   na bidhaa   mbalimbali, zao   la   dagaa   halikuainishwa, hali   inayoleta ugumu wa  kuthibiti  biashara  hiyo.

Naye, wafanyabiashara   Enock     Mussa   Pamoja   na   Kadogo Masanyiwa    kwenye Soko   la   dagaa   la   Kirumba wamekiri   madhaifu   ya   sheria   hiyo   ni   kutoainisha kipimo   cha   dagaa   na   kusababisha   malumbano   makubwa   baina   ya   wauzaji,wanunuaji na wasimamizi wa sheria.

Sheria  ya  vipimo  imeshindwa  kuainisha   zao  la  dagaa  hali  inayopelekea  uwepowa   malumbano   kwenye   usimamizi   wa   agizo   la   Serikali,   baadhi   ya wafanyabiashara, Restuta Luoga, Leonard Sprian, Jonathan   Malaba   na   William  Clemence    wametoa   mapendekezo   yao   ya   kutaka   sheria   hiyo   ifanyiwe marekebisho  ili  zao  la  dagaa  liingizwe  kwenye  sheria ili  kuleta  usimamizi  mzuriwa  agizo la  Mheshimiwa  Kassimu  Mjaliwa.

Makala  hii imefadhilwa  na  mfuko wa  Wakfu  wa tasnia ya Habari  Tanzania (TMF). Maoni  na  ushauri wasiliana  na Mwandishi wa makala hii kwa  namba 0765892256.
Soma Makala nyingine HAPA

No comments:

Powered by Blogger.