LIVE STREAM ADS

Header Ads

RAIS MAGUFULI APATA MAPOKEZI MAKUBWA MKOANI MWANZA. AWAKINGIA KIFUA MACHINGA JIJINI MWANZA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Msafara wa Rais John Magufuli, jana ukiwasili uwanja wa Mnadani wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, ukitokea mkoani Geita.
Rais Magufuli (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM wilayani Sengerema
Rais Magufuli akiwasili uwanja wa Mnadani wilayani Sengerema kuwahutubia wananchi
Rais Magufuli akiwasalimia wananchi (hawako pichani).
Kulia ni Rais Magufuli akisaini kitabu cha wageni. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Rais Magufuli akiwahutubia wananchi wilayani Sengerema 
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akitoa taarifa fupi ya maendeleo mkoani Mwanza ambapo alisema hali ya usalama iko shwari na kwamba mkoa unaendelea vyema na shughuli za maendeleo.
Mbunge wa Jimbo la Buchosa wilayani Sengerema ambaye pia ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Charles Tizeba, akizungumza katika mkutano wa Rais Magufuli mjini Sengerema. Alimuomba Rais Magufuli kuendelea kumsaidia katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami pamoja na ukamilishaji wa mradi mkubwa wa maji jimboni humo ambapo Rais aliahidi kushughulikia maombi hayo.
Mbunge wa Jimbo la Sengerema, Willium Ngeleja, akiwasalimia wananchi ambapo ambapo aliomba Rais kumsaidia kukamilisha ujenzi wa barabara ya Sengerema hadi Kamanga na utatuzi wa kero ya maji wilayani Sengerema.
Mbunge wa Jimbo la Kwimba, Shanif Mansoor, akizungumza katika mkutano huo ambapo aliomba Serikali kumsaidia fedha kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa chuo cha ufundi Veta jimbo kwake ili wahitimu waweze kunufaika na mafunzo mbalimbali ya uzalishaji mali na kwamba kiwanja kwa ajili ya ujenzi huo kilikwisha tengwa.
Mwenyekiti wa CCM wilayani Sengerema, akiwasalimia wananchi katika mkutano huo ambapo pia alimpompongeza Rais Magufuli kwa utendaji wake wa kazi pamoja na kuchaguliwa kwa kishindo kuwa Mwenyeti wa CCM Taifa.
Wakazi wa Sengerema wakifurahia hotuba ya Rais Magufuli
Ujumbe kwa Rais, ambapo alisema ameona ujumbe na atamuagiza waziri mwenye dhamana ili kufuatilia kero za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi haraka
Wakazi wa Sengerema waliofika uwanja wa Mnadani kumsikiliza Rais Magufuli
Viongozi mbalimbali akiwemo mbunge wa Sengerema (anaepiga makofi), akifurahia jambo wakati wa hotuba ya Rais Magufuli.
Viongozi mbalimbali mkoani Mwanza
Rais Magufuli akisalimiana na wananchi wa Busisi
Rais Magufuli akisalimiana na mmoja wa wakazi wa Busisi Sengerema
Rais Magufuli akiwaaga wakazi wa Sengerema
Maeneo mbalimbali ikiwemo Nyampande, Busisi wilayani Sengerema, Kigongo, Usagara wilayani Misungwi, Buhongwa, Nyegezi, Mkuyuni na katikati ya Jiji la Mwanza, umati wa wananzengo ulifurika barabarani kumlaki Rais Magufuli ambae ilimlazimu kusimama ili kusalimiana nao. 

Hali hiyo ilisababisha adha kwa baadhi ya watumiaji wa barabara kutoka na uwepo wa foleni ndefu ya magari barabarani.
---------------------------------------------------------------------------------
Rais Dkt.John Magufuli amezuia mpango wa kuwaondoa wafanyabiashara ndogondogo/machinga katikati ya Jiji la Mwanza, uliokuwa umepangwa kutekelezwa mwezi huu.

Rais Magufuli alitoa zuio hilo jana, aliposimama katika Kata ya Buhongwa Jijini Mwanza, kusalimiana na mamia ya wananchi waliojitokeza barabarani kumlaki wakati akitokea Sengerema alikokuwa na mkutano wa hadhara baada ya kuwasili wilayani humo akitokea mkoani Geita alikokuwa na mapumziko mafupi.

Aliwataka viongozi wa Jiji la Mwanza kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa na mbunge wa jimbo la Nyamagana, kushirikiana pamoja kuandaa maeneo ya kuwapeleka machinga, badala ya kuwaondoa huku kukiwa hakuna maeneo mbadala ya kuwapeleka.

Kikao cha sekretarieti ya mkoa wa Mwanza kilichoketi mwishoni mwa mwezi uliopita, kiliadhimia machinga wote kuondolewa katikati ya Jiji la Mwanza ambapo zoezi la kuwaondoa lilipaswa kuanza kutekeleza agosti 20, mwaka huu, japo mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, hakuonekana kukubaliana na maamuzi hayo kwa kuwa hakukuwa na maeneo mbadala ya machinga hao kupekelekwa.

Akiwahutubia wananchi wilayani Sengerema kwenye uwanja wa Mnadani, Rais Magufuli pia alipiga marufuku utozaji wa ushuru na kodi katika mazao ya wakulima na kutaka ushuru na kodi watozwe wafanyabiashara wakubwa.

Aidha alisema serikali yake haina mpango wa kupeleka chakula cha msaada kwenye maeneo yatakayokuwa yakipata baa la njaa badala yake kila mmoja afanye kazi ikiwemo kulima ili kukidhi mahitaji yake ya chakula kwani hata maandiko yanasema asiye fanya kazi na asile.

Rais Magufuli yuko mkoani Mwanza kwa ziara fupi ya kikazi ambapo leo anakagua na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa daraja la watembea kwa miguu la Furahisha na pia kukagua upanuzi wa ujenzi wa barabara ya Furahisha hadi Pasiansi kabla ya kuwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara utakaofanyika uwanja wa Furahisha kuanzia majira ya saa nane mchana.
Bonyeza HAPA Kwa Matukio Zaidi

No comments:

Powered by Blogger.