LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA ATAKA MSAMAHA WA USHURU KWA WAJASIRIAMALI KUTOTUMIKA KUKWEPA KODI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na Vester Joseph BMG
Halmashauri ya jiji la Mwanza imewataka wananchi kulipa kodi ikiwemo ya majengo kwa maendeleo ya nchi na haitamvumilia mwananchi yeyote atakaye kwepa kodi na kukwamisha shughuli za hamshauri hiyo.

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Jiji la Mwanza, Kiburwa Kiomoni Kibamba, amesema kodi za majengo zitasaidia kuimarisha huduma za jamii jijini humo.

Amewakumbusha pia wananchi kufuata sheria na kuacha tabia ya kukwepa kulipa kodi ili kuepukana na mkondo wa sheria huku akisisitiza juu ya msamaha wa ushuru na kodi kwa wakulima na wafanyabaishara ndogondogo uliotolewa na Rais Dkt.John Pombe Magufuli, usitumike kukwepa kodi.

Aidha Kibamba amesema zoezi la ukusanyaji wa kodi zikiwemo za leseni kwa wafanyabiashara wa maduka ambao wanakiuka sheria na taratibu zilizopo litaanza hivi karibuni.

No comments:

Powered by Blogger.