LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA LATANGAZA KIAMA KWA WADAIWA SUGU.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na James Salvatory
Shirika la nyumba la taifa NHC limewataka wadaiwa sugu wa kodi za nyumba zikiwemo taasisi za serikali na watu binafsi kulipa madeni yao yenye thamani ya shilingi bilioni 15 ndani ya mwezi mmoja kuanzia agosti 25 mwaka huu ili kuepuka adha ya kuondolewa katika nyumba walizopanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo, Nehemia Mchechu, alisema fedha hizo zitakapolipwa zitatumika kutekeleza ujenzi wa  nyumba mpya za wafanyakazi  wanaohamia mjini Dodoma na hivyo kuongeza idadi ya nyumba zinazohitajika kutokana na serikali kuhamia mjini humo.

Aliongeza kuwa kwa wale wote waliopewa notisi za kulipa kodi wahakikishe wanalipa kodi zao ndani ya muda waliopewa kinyume na hapo wataondolewa katika nyumba hizo pamoja na kuendelea na hatua nyingine za kisheria ikiwemo kukamata mali zao.

Aidha mkurugenzi huyo aliunga mkono uamuzi wa serikali kuhamishia makao makuu yake mjini Dodoma na kwamba hiyo itatoa nafasi shirika hilo kunufaika katika sekta ya ujenzi kwa kuongeza ajira, kuchochea uwekezaji na ukuaji wa viwanda vinavyohusiana na mambo ya ujenzi pamoja na kuongeza wigo wa upatikanaji wa kodi na mapato mbalimbali ya serikali.

No comments:

Powered by Blogger.