LIVE STREAM ADS

Header Ads

MLIPUKO WA PETROLI WAUA MKOANI MWANZA HUKU WENGINE WAKITIWA MBARONI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na George GB Pazzo Binagi
Mfanyabiashara mmoja mkazi wa Chifule kata ya Bukungu katika Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, amefariki dunia kwa ajali ya moto huku mwenzake akijeruhiwa vibaya.

Kamanda wa polisi mkoani Mwanza, Ahmed Msangi, amemtaja aliefariki kuwa ni Zephani Bita (42), na kwamba tukio hilo lilitokea julai 30 mwaka huu wakati marehemu akiwa na mwenzake aliefahamika kwa jina moja la Dotto ambae amelazwa katika hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.

Kamanda Msangi amesema chanzo cha moto huo ni mlipuko wa petrol uliotokea nyumbani kwa marehemu baada ya mtu mmoja kupita koridoni huku akivuta sigara wakati marehemu na aliyejeruhiwa wakimimina mafuta ya petroli kwenye dumu.

Kamanda Msangi amesema, pia moto huo ulisababisha vyumba vinne katika nyumba hiyo kutetekea pamoja na mali zilizokuwemo ambapo amesema uchunguzi wa tuki hilo bado unaendelea huku akiwaonya wafanyabishara wanaofanya biashara za mafuta petroli na diseli kinyume cha sheria kuacha mara moja.

Wakati huo huo, jeshi la polisi mkoani Mwanza linawashikiria watu watatu ambao ni Boniphace Masamaki (47), Linah Cosmas (26) na Ali Mohamed (30), wote wakazi wa Ilemela Mlimani, Manispaa ya Ilemela, kwa tuhuma za kujiunganishia umeme kinyemela jambo ambalo ni kinyume cha sheria na taratibu za Shirika la Umeme nchini Tanesco.

Watuhumiwa hao walikamatwa baada ya msako mkali uliofanywa julai 31,2016 na ambao bado unaoendelea uliofanywa na maofisa wa Tanesco pamoja na polisi ambapo Kamanda Msangi amewaonya wananchi kuacha tabia hiyo kwani licha ya kutiwa nguvuni pia ni hatari kwa usalama wao.

No comments:

Powered by Blogger.