LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWALIMU WA SHULE YA SEKONDARI NYAKABUNGO JIJINI MWANZA ATUHUMIWA KUFANYA MAPENZI NA WANAFUNZI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Displaying Screenshot_2016-08-25-21-24-06-1.png
Na Vester Joseph BMG
Mmoja wa waalimu wa shule ya sekondari Nyakabungo iliyopo Jijini Mwanza, wanatuhumiwa kujihusisha na mahusiano ya kimapenzi na baadhi ya wanafunzi shuleni hapo.

Hali hiyo imewafanya baadhi ya wazazi wa wanafunzi wanaosoma katika shule hiyo nkuiomba serikali kuwachukulia hatua kali waalimu watakaobainika kujihusisha katika vitendo hivyo vichafu.

Habari za kuaminika kutoka shuleni hapo zimetanabaisha kwamba kuna wanafunzi wa kike wapatao watano wa kidato cha kwanza ambao wamebainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mmoja wa walimu ambaye alikuwa katika mafunzo ya vitendo katika shule hiyo.

Miongoni mwa wazazi ambao watoto wao wanadaiwa kuhusika na tuhuma hizo ambao wamefika katika shule hiyo, wamewasilisha kilio chao kwa serikali na kutaka tabia hiyo ikomeshwe mara moja.

Akizungumza na BMG, Mkuu wa shule hiyo,  mwalimu Boniface Mjuli, alisema amelazimika kuwaita wazazi hao na kuwataka kwenda shuleni hapo na vipimo vya afya za watoto wao ikiwemo kubaini hali ya mimba, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mzazi mmoja ambaye binti yake anahusika na mahusiano ya kimapenzi na mwalimu huyo ambaye kwa sasa anafanyiwa uchunguzi.

Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo wamelaani kitendo cha mwalimu huyo ambaye ni mwanafunzi kutoka chuo cha Tumaini tawi la Makumila kulalamikiwa kujihusisha na vitendo vya mapenzi na wananafunzi wa shule hiyo.

Taarifa ambazo BMG imezipata zinaeleza kwamba tayari kamati ya nidhamu ya shule hiyo inafanya uchunguzi kuhusu suala hilo kwa ajili ya hatua zaidi za kinidhamu.

No comments:

Powered by Blogger.