LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAMILIKI WA VIWANDA VYA KUCHAMBUA ZAO LA PAMBA WATAKIWA KUTENGA MBEGU BORA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Shaban Njia, Kahama
WAMILIKI wa Viwanda vya kuchambulia Pamba Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wametakiwa kutenga mbegu zilizo bora zilizotoka katika maeneo ambayo hayana ugonjwa wa zao hilo kwa ajili ya kuzigawa kwa wakulima katika msimu ujao wa Kilimo cha zao la Pamba mwaka 2016/2017.

Mkurugenzi wa huduma za usimamizi wa zao la Pamba nchini (DRS) James Shimbe aliyasema hayo kwa nyakati tofauti wakati akikagua mbegu za Pamba kwa wamiliki wa Viwanda vya kuchambulia Pamba vya Kahama oil Mil na Kahama cotton Kampany Limited (KCCL) vya Mjini hapa.

Shimbe alisema kuwa katika msimu ujao wa Kilimo cha Pamba lazima wakulima wa zao hilo waweze kupata mbegu kwa wakati hali ambayo inaweza kusadia kwa wakulima kulima zao hilo kwa muda uliopangwa tofauti na awali mbegu hizo zilipokuwa zikichelewa kufika kwa wakulima.

Alisema  kwa sasa Wamiliki wa Viwanda vya kuchambulia Pamba ndio wanatakiwa kusambaza mbegu kwa wakulima lakini kabala ya kuanza zoezi hilo kitengo cha udhibiti wa Mbegu bora (TOSK) kitahakikisha kuwa kinazikagua mbegu hizo kabla ya kuwafikia wakulima wa zao hilo.

Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa toski ambao ndio wasimamizi wakubwa wa Mbegu wapo tayari katika kukagua mbegu hizo ambazo hufungwa kwa tani 25 kila fungu lambegu hizo huku akisisitiza kuwa zoezi la kuanza kusambaza mbegu hizo unaweza kuanza mwezi septemba mwaka huu kabla ya mvua kuanza.

Alisema kuwa kwa msimu huu wa kilimo cha zao la Pamba lazima wakulia waweze kupata mbegu ambazo zitaweza kuota na kuondoa malalamiko yaliokuwepo katika msimu uliopita kwa Wakulima kuhusu kuwepo kwa mbegu ambazo hazikuweza kuota hali ambayo iliwafanya kutofikiria tena kulima zao hilo.

Kwa upande wake Maeneja uzalishaji wa Kiwanda cha kuchambulia Pamba cha Kahama Oil Mil (KOM) Bryson Edward alisema kuwa kiwanda chake tayari kimetenga asilima 25 za mbegu hadi kufikia sasa na kuongeza kuwa kwa sasa wanasubiri maelekezo  kutoka katika bodi ya Pamba hapa nchini ili kuanza kugawa mbegu kwa wakulima.

Aidha Edward alisema kuwa katika msimu ulipita wa Pamba wameweza kupata Pamba iliyosafi tofauti na miaka mingine ingawa mavuno yalikuwa ni machache nakuongeza kuwa Kampuni yake ilikuwa na malengo ya kununua kiasi cha tani milioni 13 lakini kutokana na pamba kuwa chache walifanikiwa kupata kiasi cha tani milioni sita tuu.


Pia kutoka na hali hiyo Meneja huyo uzalishaji wa Kiwanda cha Kahama Oil Mil aliitaka Serikali kuhakikisha kuwa  inadhibiti ubora wa zao la Pamba kutoka katika ngazi za Wakulima hali ambayo itaweza kurudisha Ubora wa zao hilo kama ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

No comments:

Powered by Blogger.