LIVE STREAM ADS

Header Ads

NINI LENGO LA SERIKALI KUKATA RUFAA JUU YA KESI YA KUPINGA NDOA ZA UTOTONI?

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

"Mahakama Kuu imetoa hukumu leo ya ndoa za utotoni, na kusema

vifungu vya 13 na 17 viko kinyume na Katiba na kutoa umri wa miaka 18 kuwa umri wa kuolewa kwa mtoto wa kike. Tunafuraha sana, huu ni ushindi kwa wasichana wote wa Tanzania. Big congrats to our ED @rebecagyumi who filed the petition, and
@advocate_jebra our counsellor". Julai 08,2016 Msichana Initiative waliandika hivyo kupitia ukurasa wao wa facebook.


Siku chache baada ya ushindi huo, Serikali kupitia kwa Mwanasheria wake Mkuu imewasilisha mahakamani ombi la kukata rufaa ili kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es salaam kupinga ndoa za watoto chini ya miaka 18.

Hukumu ya kesi hiyo ilitaka kufutwa kwa kifungu cha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 kinachoruhusu mtoto wa kike kuolewa hata akiwa na umri kuanzia miaka 14 kwa idhini ya wazazi/walezi.

Awali katika kesi hiyo iliyofunguliwa na watetezi wa haki za watoto kutoka taasisi ya "Msichana Initiative" walitaka umri sahihi wa ndoa kwa wasichana na wavulana kuwa miaka 18.

Kumbuka sheria ya ndoa ya mwaka 1971 inaeleza bayana kwamba, wavulana wanaweza kuoa wakiwa na umri wa kuanzia miaka 18 huku wasichana wakiolewa wakiwa na umri kuanzia miaka 15.

BMG tunahoji nia ya serikali juu ya rufaa hiyo ama inataka ndoa za utotoni ziendelee kuwepo ama lengo lake hasa juu ya rufaa hiyo ni nini? Kumbuka mbali na madhira ya kiafya, pia wasichana wengi wamekuwa wakipitia manyanyaso mengi ikiwemo utumwa wa kingono kutokana na hizi ndoa za utotoni.

No comments:

Powered by Blogger.