LIVE STREAM ADS

Header Ads

KWA YA HAVILLAH GOSPEL SINGERS KUTOKA EAGT LUMALA MPYA JIJINI MWANZA KUTUMBUIZA NCHINI KENYA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Kwaya ya Havillah Gospel Singers ya Kanisa la EAGT Lumala Mpya lililopo sabasaba Jijini Mwanza, imepata mwaliko wa kwenda kuhudumu nchini Kenya katika kongamano lililopewa jina la “International Burning Fire Conference” litakalofanyika Jijini Nairobi.

Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika Agost 07 hadi 14 mwaka huu ambapo limeandaliwa na Kanisa la Revival Sanctuary of God Church na wahudumu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Kenya wanatarajiwa kuhudumu katika kongamano hilo.

Waimbaji wa kwaya hiyo ya Havillah wametoa shukurani zao za dhani kwa kupata kibali cha kualikwa katika kongamano hilo na wametoa shukurani zao za dhati kwa Mchungaji wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya, Dkt.Daniel Moses Kulola, Mama Mchungaji, Mercy Kulola na waumini wote wa kanisa hilo kwa Baraka zao wakati wakijiandaa na safari ya kuelekea nchini Kenya itakayoanza wikendi ijayo.

No comments:

Powered by Blogger.