LIVE STREAM ADS

Header Ads

SHIRIKA LA RELI NCHINI TRL LATOA BEI ELEKEZI KWA ABIRIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory - BMG Dar
Shirika la reli nchini (TRL) limetoa nauli elekezi ya shilingi 600 kwa wasafiri wanaotumia usafiri wa reli kwa wakaazi wa jiji la Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi wa shirilika hilo Nghwani Mdema amesema nauli hiyo elekezi ya shilingi 600 itaanza kutozwa baada ya wiki mbili kuanzia leo.

"Nauli hii itaendana sambamba na ile ya wanafunzi 100 baada ya mamlaka ya usafirishaji majini na nchi kavu SUMATRA kufanya ukokotozi juu ya gharama ya nauli ya usafiri huu,"Alisema Mdema.

Mdema alisema kuwa katika kuboresha huduma ya shirika hilo linatarajia kuongeza mabehewa mawili ambapo hapo awali yalikuwa yakitumika mabehewa kumi na nane na hivyo kuongeza hayo kufikikia mabehewa ishirini.

"Kwa kipindi cha wiki moja shilika hili lilikuwa likitoa huduma kwa wananchi na wakaazi wa Dar es salaam awamu mbili asubuhi na jioni bila kutoza malipo

yeyote"Aliongeza Mdema.

No comments:

Powered by Blogger.