LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO KUWA MGENI RASMI KWENYE MBIO ZA ROCK CITY MARATHON 2016.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi  katika mashindano ya Rock City Marathon yanayotarajia kufanyika semptemba 25 mwaka huu,na kutimua vumbi katika uwanja wa CCM Kirumba wilayani Ilemela mkoani hapa.

Haya yalibainishwa jana  na Ofisa Habari na Mawasiliano mkoa Mwanza Atley Kuni wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Kuni alisema, mbali na mashindano hayo kusaidia kuimarisha afya na kuinua vipaji vipya, pia yanalengo la kukuza Utalii na kupiga vita ujangili kupitia michezo hiyo.

Pia alisema, mbio hizo zimegawanyika katika makundi manne  ikiwemo kilomita 21, km 5  kwa wenye ulemavu wa ngozi, km 3   kwa wazee kuanzia miaka 55 na  km 2 kuanzia miaka 7 hadi 10.

Hata hivyo aliwaomba wananchi, kujitokeza kushiriki  katika mashindano hayo, kwani mkoa inayachukulia kwa uzito ni muhimu kwa maendeleo ya utalii,uchumi, biashara na michezo Mwanza.

Kwa upande wake Ofisa Michezo Mkoa wa Mwanza James William alisema, zawadi mbalimbali zitatolewa kwa washiriki watakaoshika nafasi ya kwanza mpaka kumi.

Aidha aliwaomba, waandishi wa habari kujitokeza katika mashindano hayo, pia na jamii ya mikoa jirani ya Geita,Simiyu na Shinyanga kushiriki kwenye mbio hizo.

No comments:

Powered by Blogger.