LIVE STREAM ADS

Header Ads

ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 300 ZAPATIKANA KWENYE HARAMBEE YA KUCHANGIA MADAWATI CHATO MKOANI GEITA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na Vester Joseph
Wakati serikali ikihakikisha elimu inatolewa bure hapa nchini, Wilaya ya Chato mkoani Geita imechangia shilingi Milioni 305 kwa ajili ya utengenezwaji wa madawati kwa shule zote za wilayani humo.

Uchangiaji huo ulifanyaika katika harambee iliyoandaliwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa jimbo la Chato, Dk.Medard Kalemani, iliyofanyika hivi karibuni jijini Mwanza.

Diwani kata ya Muganza iliyoko Wilayani Chato, Emanueli Mwita Nyamranga, ameiambia Binagi Blog_BMG kwamba fedha zilizopatikana katika harambee hiyo zitatengeneza madawati 6,100 huku mahitaji ya madawati katika wilaya hiyo yakiwa ni elfu 10 kwa shule zote za wilaya hiyo.

Nyamranga amewataka wananchi wa Wilaya ya Chato kuendelea kujitokeza kuchangia maendeleo ya Wilaya hiyo ili kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano ya Dk.John Pombe Mgufuli.

“Tumefanya harambee ya kuchangia maendeleo ya Wilaya yetu ya Chato katika elimu ambapo tumepata shilingi Milioni 305,721,500 ambazo zitatumika kutengeneza madawati 6,100 kati ya mawadati elfu 10 yanayohitajika katika Wilaya yetu;

Pamoja na kupata fedha hizi bado tunawaomba wananchi kuendelea kuchangia utengenezaji wa madawati ili kuhakikisha tatizo la madawati linaisha katika Wilaya yetu na kuunga mkono jitihadi za serikali ya awamu ya tano". Alisema Nyamranga.

No comments:

Powered by Blogger.