LIVE STREAM ADS

Header Ads

IDADI YA MAUZO KWENYE SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM YAPANDA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for IMAGE SOKO LA HISA LA DAR ES SALAAM
Na James Salvatory - BMG Dar
Idadi ya mauzo katika soko la hisa la Dar es salaam Stock Exchange (DSE), imeongezeka kwa asilimia 73% na kufikia  tzs 3.8 bilioni kutoka shilingi bilioni 2.2 huku mtaji wa makampuni ya ndani ukishuka kwa asilimia 1.6 kutoka trioni 8.3 hadi trioni 8.2.

Akizungumza na waandishi wa Habari jana jijini Dar es salaam Meneja miradi Masoko na Biashara Patrick Mususa amesema kuwa hali hiyo imechangiwa na shughuli mabalimbali za manunuzi na kuuza hisa zao baada ya soko hilo kukuza uelewa ikiwemo kutumia vyombo vya habari juu ya umuhimu wa hisa katika kukuza uchumi.

"Wakati huo Makapuni yanayoongoza katika kuuza hisa katika soko lahisa ni pamoja CRDB kwa 28.66% ,DSE 22.39% huku kampuni ya sigara nchini ya TCC ikishika nafasi ya tatu kwa 21.87%  kwa kununuliwa hisa zake,"Alisema Mususa.

Mususa alisema kuwa wakati mauzo ya hisa yakiongezeka kwa asilimia 73 sekta ya viwanda imeshuka kutokana na kupungua kwa kaunta ya kampuni ya bia nchini (TBL) kwa asilimia 2.6 huku Sekta ya kibenki imeonekana kushuka kutokana na ongezeko la hisa katika kaunta ya soko la hisa kushuka kwa
asilimia 0.82.

"Sambamba na hilo pia katika soko letu kumekuwa na mwitikio mkubwa kwa wanafunzi hasa katika kipindi cha mwaka jana ambapo wanafunzi wengi walijitokeza kununua hisa kwa asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka huu ambapo mkoa wa Arusha ndio umekwa ukiongoza kwa wanafunzi kuwekeza kupitia soko la
Hisa,"Aliongeza Mususa.

No comments:

Powered by Blogger.