LIVE STREAM ADS

Header Ads

WILAYA YA UKEREWE MKOANI MWANZA YAPATA GARI LA ZIMAMOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying DC 2.JPG
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe Estomihn Francis Chang’ah akifungua mlango wa gari ya zimamoto na uokoaji aliyokabidhiwa na kamanda wa zimamoto mkoa wa mwanza Ili kusaidia kudhibiti maafa ya moto yanayoweza kujitokeza wilayani humo.

Idara ya Zimamoto na Uokoaji Wilaya ya Ukerewe imepokea gari moja la kuzimia moto ili kudhibiti maafa ya moto na yanayoweza kutokea katika kisiwa cha Ukerewe.

Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomihn Francis Chang’ah, ameshukuru serikali kupitia Idara ya zimamoto Mkoa wa Mwanza kwa kusikia kilio na haja ya wananchi wa Ukerewe na kuwezesha kupatikana kwa gari hilo la zimamoto. Gari hilo lina vifaa vyote vya uokoaji.

Ameyasema hayo katika makabidhiano ya gari hilo ambapo amewataka wananchi kutokua na shaka kwani kikosi cha zimamoto Wilayani Ukerewe kipo kamili na kina mbinu zote za uokoaji. 

Nae Kamanda Zimamoto Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Andrew Mbate, amekabidhi gari hilo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe na kumshukuru kwa ahadi yake ya kuhakikisha kuwa Tanki la Maji ambalo litawezesha litatumika kujaza maji kwenye gari hilo la kuzimia moto.

"kwa sasa Wilaya ya Ukerewe limekabidhiwa na litaanza kutumika kudhibiti moto ya Awali na baadae kamishina wa Zimamoto Mkoa ataleta gari kubwa zaidi hvyo kuwezesha kukidhi mahitaji ya eneo kubwa la Kisiwa cha Ukerewe,"Alisema Mbate

Makabidhiano hayo yalifanyika na hadi sasa Kikosi cha Zimamoto Ukerewe kina Ukosefu wa Tanki kubwa la maji yatakayotumika kujaza gari hilo.

Katika kushughulikia changamoto hiyo ya ukosefu wa tanki la maji mkuu wa wilaya hiyo Chang’ah ameahidi kuwashirikisha wadau wa maendeleo wilayan Ukerewe ili kuweza kufanikisha upatikanaji wa tanki hilo Muhimu katika shughuli ya Zimamoto na uokoaji.


Naye CPL.Nyanzala Ndutu kiongozi wa Kikosi cha Zimamoto Ukerewe ameshukuru Idara ya Zimamoto Mkoa na Serikali kwa kuwapatia kitendea kazi hiko Muhimu na kuahidi kukitunza na kukitumia katika kukabiliana na majanga yote ya moto yanayoweza kujitokeza ndani ya Wilaya.
Displaying DC na ANDREW MBATE.JPG
Kamanda wa kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Andrew J. Mbate (kushoto), akimkabidhi funguo za gari la kuzimia moto Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Estomihn Francis Chang’ah (kulia) ili kudhibiti maafa ya moto na yanayoweza kutokea katika wilaya hiyo.
Imeandaliwa na Stephen Msengi Afisa habari halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe.

No comments:

Powered by Blogger.