LIVE STREAM ADS

Header Ads

ILEMELA WATAKIWA KUEPUKANA NA UHALIBIFU WA MIUNDOMBINU YA BARABARA KWA MAKUSUDI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for BARABARA ILEMELAJudith Ferdinand, Mwanza
Wananchi   wa Kata ya Ilemela mkoani Mwanza, wametakiwa kuacha tabia ya kuchimba mchanga katika  hifadhi za barabara pamoja na kutupa takataka ovyo, ili kuepukana na uharibifu wa miundombinu hiyo hususani nyakati za mvua za masika.

Wito huo ulitolewa juzi na diwani wa Kata ya Ilemela, Willbard Kilenzi, wakati akizungumza na BMG ofisini kwake mkoani hapa.

Kilenzi alisema, wananchi waache tabia ya kuchimba mcha nga maeneo ya barabara kwani  yanasababisha mmomonyoko wa udongo pamoja na utupaji takataka katika mitaro inayopelekea maji kukosa muelekeo na kupita katikati ya barabara ambao ndio chanzo cha miundombinu hiyo kuharibika hasa kipindi cha masika.

Alisema hii ni kutokana na   serikali  kufanya ukarabati wa  barabara zilizoharibiwa na mvua  kipindi cha masika kwa kiasi kikubwa katika kata hiyo, licha ya changamoto zinazojitokeza kwenye baadhi ya maeneo.

Pia alisema  serikali kupitia Mfuko wa Dharura wa  Matengenezo ya Barabara( zilizokua zimeharibiwa na mvua kipindi cha masika),imetoa jumla ya shilingi milioni 240, kwa ajili ya ukarabati wa  barabara mbili ikiwemo barabara inayo anzia Ilemela Msikitini  kupitia mahakamani mpaka Wedi inayogharimu milioni 61, huku barabara inayoanzia  dampo inapita shule ya sekondari Kiseke mpaka Green View inaumbali wa kilomita 2.5 na kugharimu milioni 179.

Hata hivyo alisema barabara hizo zitengenezwa kwa kiwango cha moramu, kutengeneza mitaro  sambamba na kujenga madaraja makubwa ambayo yatasaidia kupitisha maji kwa urahisi bila kukwama.

Vilevile alisema miradi hiyo ya utengenezaji wa barabara hizo ulianza mwezi Augusto na wanatarajia kukamilika oktoba mwaka huu.

Aliongeza kuwa barabara hizo zimejengwa kwa juhudi za pamoja za Diwani, Mbunge Angelina Mabula, halmashauri ya Manispaa ya Ilemela likiwemo baraza la madiwani Mkurugenzi John Wanga.

No comments:

Powered by Blogger.