LIVE STREAM ADS

Header Ads

WANANCHI WATENGENEZA MAKABURI HEWA KULIPWA FIDIA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Image result for PICHA ZA MAKABURINa Happy Severine, Simiyu,
Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wananchi Mkoani Simiyu ambao wamekuwa wakipitiwa na miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami, wanadaiwa kubuni njia za kulipwa fidia kwa kutengeneza  makaburi hewa.

Miradi hiyo ambayo ipo chini ya wakala wa Barabara Mkoani hapa (TANRODS), inaelezwa kuwa pindi miradi hiyo inapoanza ujenzi wake wananchi wengi ujenga ubuni na kutengeneza  makaburi hewa na kudai kuwa  barabara imeyafuata makaburi hayo.

Hayo yalielezwa jana na Meneja wa wakala wa Barabara Mkoa Albert Kent wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani humo, kilichofanyikia katika kanisa Katoliki Mtakatifu John Mjini Bariadi.

Kent alieleza kuwa jumla ya makaburi 4 yaligundulika kuwa hewa katika mradi ambao umemalizika ujenzi wake wa Lamadi-Bariadi, ambapo ni kaburi moja tu ambalo liligundulika kuwa  ni la kweli .

Alisema katika makaburi hayo tayari wamiliki walikuwa wamelipwa fidia, ambapo walipata taarifa kutoka kwa raia wema na kuelezwa kuwa baadhi ya makaburi ni hewa.

“ tulipopata taarifa tukawataka hao wananchi ambao tayari tulikuwa tumewalipa, ukawataka kurudisha pesa hizo…walipokataa tukawaita viongozi wa serikali za vijiji na kata…tukawaamuru kufukua makaburi hayo 4 kati ya 5 yalikuwa hewa, tukaridishiwa pesa zetu” Alisema Kent

Aidha aliongeza kuwa katika Mradi mpya wa ujenzi wa barabara ya Maswa-Mwigumbi inayojengwa kwa kiwango cha lami, jumla ya makaburi 5 yalikutwa hewa kati ya 6 yaliyokuwa yalipiwe fidia.

Aliongeza kuwa  katika makaburi hayo kiasi cha shilingi Milioni sita kilikuwa kimetengwa kwa ajili ya kulipia fidia, lakini baada ya kuchunguza Tanroads ililipa shilingi 500,000 tu na pesa zilizobaki kurejeshwa serikalini.

“ baada ya kugundua kuwa watu wanatengeneza makaburi hewa katika mradi wa Lamadi-Bariadi, katika mradi wa Mwingumbi-Maswa kabla hatujalipa tulikuwa tunawalazimisha wamiliki wafukue kwanza ndiyo tuwalipe” Alisema Kent

Alieleza katika zoezi la kuhakiki kama ni makaburi ya kweli walikuwa wakiambatana na viongozi wa vijiji, ambapo wamiliki walikuwa wakiamuliwa kufukua wao wenyewe kabla ya kulipwa pesa zao.

Hata hivyo wakala huo unatemegemea kutumia zaidi ya shilingi Bilioni 11 katika mwaka wa fedha 2016/17 katika miradi mbalimbali ya barabara Mkoani hapa.

No comments:

Powered by Blogger.