LIVE STREAM ADS

Header Ads

KAMPUNI YA MABATI YA ALAF YAWAHIMIZA MAFUNDI UJENZI MKOANI MWANZA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIMAFUNZO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Mafundi ujenzi mkoani Mwanza, watakiwa kuchangamkia fursa za mafunzo, yanayotolewa na mashirika mbalimbali nchini ili kuongeza ujuzi na kuboresha kazi zao.

Wito huo ulitolewa  jana Jijini Mwanza na Mhandisi wa kampuni ya mabati ya Alaf, Daudi Kidyamali, wakati akizungumza na BMG kuhusiana na fursa ya kimafunzo ambayo hutolewa mara kwa mara na kampuni hiyo.

Kidyamali alisema, ni vema mafundi  wakawa na utaratibu wa kufuatilia mafunzo yanayotolewa na kampuni  mbalimbali zinazojishughulisha  na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi kwa lengo la kuwajengea uwezo na kufanya kazi zao kwa ufanisi.

“Nawaomba  mafundi  ujenzi kujijengea mazoea ya kuhudhuria mafunzo yanayotolewa na kampuni mbalimbali zinazojishughulisha na utengenezaji wa vifaa vya ujenzi, ili kuongeza  ujuzi  na ufanisi katika kazi zao," alisema Kidyamali.

Pia alisema, kupitia mafunzo yanayotolewa na kampuni hizo, yanawasaidia mafundi hao kuboresha na kuwa wabunifu katika kazi zao, kwani wengi wao hawajasomea  na hawana utaalamu wa fani hiyo.


Hata hivyo alisema, kupitia shirika hilo, wanawaelekeza mafundi namna ya uezekaji na utumiaji vifaa bora,ambavyo vitafanya kazi yake iwe bora na kumjengea uaminifu kwa wateja.

No comments:

Powered by Blogger.