LIVE STREAM ADS

Header Ads

KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU CHATAKA ADHABU KALI ITOLEWE KWA WANAOSHINDWA KUTOA MALEZI BORA KWA WATOTO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Wafanyakazi wa LHRC wakijumuika na watoto wanaolelewa katika Makao ya taifa ya watoto wenye shida Kurasini jijini Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya kusherehekea miaka 21 tangu kuanzishwa kwake.
Na Dotto Mwaibale
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Dk. Helen Kijo-Bisimba (katikati) akiwasaidia watoto kukata keki kusheherekea miaka 21 ya LHRC.
Ofisa Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida Kurasini, Beatrice Lawrance, akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo.
                                                    *******************************
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)  kimeiomba serikali kupitia wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto, pamoja na na Wizara ya Katiba na Sheria, kufanya marekebisho ya Sheria ya Mtoto  na kutilia mkazo malezi bora ya watoto ikiwemo kuweka kipengele kitakachotoa  adhabu kali  kwa familia itakayo shindwa kutoa malezi bora kwa watoto au kutelekeza familia.

Akizungumza katika maadhimisho ya  miaka 21 ya kituo cha sheria na haki za binadamu, yaliyofanyika katika Makao ya Taifa ya Watoto wenye shida kilichopo Kurasini, Temeke Jijini Dar es salaam,  Mkurugenzi Mtendaji wa  kituo hicho Dk. Helen Kijo-Bisimba alisema kuboreshwa kwa sheria hizo kutasaidia kupunguza wimbi la watoto wasio na makao maalumu  wanao zagaa kuomba omba mitaani, na ameitaka jamii  kushiriki katika kutatua tatizo la watoto wa mitaani linalozidi kushika hatamu kila siku.

Ofisa Mfawidhi wa kituo  hicho,  Beatrice Laurence  ame kishukuru kituo cha sheria na haki za Nina damu kwakuona umuhimu wa kutoka misaada katika kuwa saidia watoto wanao lelewa  hapo  nakuwataka watanzania wengine  badala ya kuelekeza nguvu zao  pekee kwa wathirika wa tetemeko huko Kagera  kuwa kumbuka na  watoto yatima kwani nao  wanayo kahitaji ya kibinadamu.

Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kilianzishwa Septemba 26, 1995 kwa lengo la kufanya utetezi kwa watu wenye uhitaji sambamba na kulinda haki za binadamu nchini.

No comments:

Powered by Blogger.