LIVE STREAM ADS

Header Ads

KIWANDA CHA SARUJI CHAIPIGA TAFU SHULE YA SEKONDARI YA ILBORU YA ARUSHA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

KIWANDA Cha Saruji Cha Simba (Simba Cement) cha Tanga, kimeipa shule ya Sekondari ya Ilboru Secondary School ya Arusha mifuko 400 ya saruji yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa ujenzi wa vymba vya madarasa.

Akizungumza wakati wa halfa fupi ya makabidhiano leo, Mkuu wa Idara ya Rasilimaliwatu kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Diana Malambugi, alisema msaada huo umetolewa ili kupunguza changamoto za vyumba vya madarasa kwa shule hiyo.

Alisema msaada huo utapunguza uhaba wa vyumba vya madarasa na kutoa wito kutumika kama ilivyokusudiwa na kuiagiza kamati ya shule kuhakikisha mifuko hiyo inatumika ipasavyo.

‘Mifuko hii ya saruji itapunguza changamoto inayoikabili shule yako  ikiwemo vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za walimu, sera yetu moja wapo ni hii ya elimu” alisema Malambugi.

Alimtaka mwalimu huyo na kamati yake ya shule kuitunza mifuko hiyo ya saruji na kumhakikishia kuisaidia pale ambapo kutakuwa na uhitaji na kuwataka wadau wengine wa elimu kusaidia sekta ya elimu zikiwemo kuondosha changamoto za uhaba wa madawati na vyumba vya madarasa.

Kwa upande wake, mwalimu mkuu wa shule ya Ilboru sekondari school ,  Julias Shulla, alikishukuru kiwanda hicho na kusema kuwa msaada huo utatumika kama ilivyoombwa.

Alisema shule yake inakabiliana na changamoto nyingi zikiwemo uhaba wa vyumba vya madarasa pamoja uhaba wa vifaa vya maabara hivyo kuwataka wadau wa elimu kuisaidia.

‘Tunakishukuru kiwanda cha saruji cha simba kwa moyo wao waliounyesha kwetu, kwa fadhila hii tunawaahidi kuwa tutaitumia saruji kama tulivyoiomba” alisema Shulla.

Alisema mifuko hiyo itapunguza kwa kiasi kikubwa  changamoto ambazo shule yake inakabiliana nazo na kusema kuwa msaada huo ni faraja kwao na wanafunzi wa shule yake.



Mkuu wa Idara ya Rasilimawatu kiwanda cha Sauji cha Simba Cement cha Tanga, Diana Malambugi, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya milioni 4.8 kwa mwalimu mkuu shule ya Sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla  ikiwa ni ujenzi wa vyumba vya madarasa.nyuma kulia ni Mkuu wa fedha Pieter Jaggar na kushoto ni Emmanuel Jonas mhasibu.
  Mhasibu wa kiwanda cha Saruji cha Simba Cement, Emmanuel Jonas, akimkabidhi mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Iboru ya Arusha, Julias Shulla mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 kwa ajili ya ujenzi wa vymba vya madarasa, nyuma ni mkuu wa fedha, Pieter Jaggar.


 Afisa Uhusiano kiwanda cha Saruji cha Simba Cement cha Tanga, Mtanga Nnour, akimkabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shlingi milioni 4.8 kwa mwalimu  mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla, ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa. Nyuma ni mkuu wa fedha, Pietre Jaggar.
 Mkuu wa fedha kiwanda cha saruji cha Simba Cement, Pieter Jaggar, akimabidhi mifuko ya saruji 400 yenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4.8 mwalimu mkuu wa shule ya sekondari ya Ilboru ya Arusha, Julias Shulla ikiwa ni kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa, kulia ni meneja usambazaji na ugawaji, Samwel Shoo, nyuma kulia ni Afisa Uhusiano , Nour Mtanga  na mkuu wa Idara ya Rasilimawatu, Diana Malambugi.
Imeandaliwa na Mtandao wa Tanga Kumekucha

No comments:

Powered by Blogger.