LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAN TRADE yahimiza ushirikiano na TCCIA Maonesho ya Biashara ya Afrka Bashariki

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Mwenyekiti waTCCIA mkoani Mwanza, Eribarick Mmari

Judith Ferdinand, Mwanza
Chama cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda na kilimo (TCCIA) mkoa wa Mwanza, ambao ndio waandaaji wa maonyesho ya Biashara ya Afrika Mashariki, wameshauri kushirikiana na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TAN TRADE), katika kuandaa maonyesho yajayo, ili yawe yenye tija na hadhi.

Wito huo ulitolewa jana na Afisa Biashara Mwandamizi Masoko ya nje wa TAN TRADE, Getrude Ng'weshemi, wakati akizungumza katika maonyesho hayo, yanayofanyika katika uwanja wa soko la kimataifa la Rocky City Mall mkoani hapa.

Ng'weshemi alisema, TCCIA inatakiwa kuboresha maonyesho hayo kwa kushirikiana na mamlaka hiyo, ambayo ina wataalamu wa masuala la upangiliaji wa mabanda katika maonyesho, ili yawe na tija sambamba na kuendana na hadhi ya Afrika Mashariki.

"Maonyesho yalianza vizuri lakini tatizo ni kuchelewa kwa washiriki kwani wengine wanafika siku ya nne,pamoja na ukosefu wa wataalamu watakao panga mabanda ya bidhaa ya aina moja sehemu yake, ili yaendane na hadhi ya Afrika Mashariki, hivyo sisi TAN TRADE tupo tayari kushirikiana nao, kwani malengo yetu yanafanana katika kuinua uchumi binafsi na taifa," alisema Ng'weshemi.

Pia alisema, TCCIA wanatajiwa kuongeza ushirikiano na wafanyabiashara pamoja na makampuni yaliyopo katika nchi za ukanda huo, sambamba na kuyatangaza ili maonyesho yajayo yawe na washiriki wengi zaidi na wananchi wajitokeze kwa wingi.

Hata hivyo alisema, kupitia maonyesho wafanyabiashara wanapata fursa ya kujifunza,ushauri, kutangaza bidhaa na kuuza pamoja na kusogea katika maonyesho mengi yanayofanyika nchi nyingine na kusogea kwenye soko zaidi.

"Kupitia maonyesho wafanyabiashara wanapata fursa ya kwenda katika maonyesho mengine na kusogea zaidi katika soko kama vilevile Mwatex na Nyanza Works Roads kupitia maonyesho haya, yamepatabmualiko wa kushiriki maonyesho nchini Kenya yatakayo fanyika semptemba 29 hadi Oktoba 02, 2016" alisema Ng'weshemi.

Aidha aliwaomba TCCIA kuweka hoteli chache zenye uwezo wa kutoa huduma bora,pamoja na serikali kuwasaidia kupata eneo la kudumu kwa ajili ya maonyesho hayo, ili kuongeza washiriki zaidi na kuhamasisha wananchi.

No comments:

Powered by Blogger.