MADEREVA WA TAX, BAJAJI NA BODABODA WATAKIWA KUBADILI MFUMO WAO WA KAZI.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory Bmg Dar
Wafanyabiashara wa Taxi, Bajiji na Bodaboda wametakiwa kubadilisha mfumo wao wa kibiashara na kuwa wa kisasa zaidi ili kuendana na ushindani uliopo.
Mkurugenzi wa usafirishaji wa kampuni ya Fasta fasta, Mohamed Shariff, jana alisema lengo la kampuni yao ni kuufanya usafiri wa jiji la dar es salaam kuwa wa kisasa huku madereva wa vyombo hivyo wakiunganishwa na wateja kwa njia ya mtandao.
Alisema huduma hiyo ya usafiri inayotumia Teknolojia hutoa uhakika wa usafiri muda wowote mahali popote, hupunguza gharama za ziada, huduma inakufuata ulipo kwa njia ya mtandao vile vile usalama wa abiria kwani abiria anakuwa na taarifa za dereva wake.
"Huwa tunaitisha mkutano na madereva wa boda boda, bajaji na taxi kisha tunaongea nao ili kuwaweka kwenye mfumo wetu na wanapokuwa wanafanya kazi sisi tunachukua asilimia 15 tu ya pesa inayopatikana”, alisema Shariff.
Aliongeza kuwa mbali na mfumo huo kuwainua madereva kibiashara bado watapata fursa ya kujifunza masuala mbali mbali ya usalama barabarani pia kuongeza uhakika wa usalama kwa watumiaji kwani fasta fasta itakuwa na taarifa kamili za madereva wote iliowasajili.
Kaimu Kamanda Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi wa Polisi Fortunatus Musilimu alisema uwekezaji huo unaoendelea utasaidia kupunguza ajari za usalama barabarani na kurahisisha upatikanaji wa taarifa za madereva wote.
“Madereva wengi wa Bodaboda, Taxi na Bajaji hawana vituo vya kazi hivyo hata taarifa zao huwa hazipatikani kiurahisi wanaposababisha ajali na kufanya vitendo vya uharifu lakini wakishajiunga na mfumo huu itakuwa ni rahisi kuwajua,”alisema Musilimu.

No comments: