WAJASIRIAMALI MKOANI MWANZA WAPATIWA MAFUNZO YA KUBUNI BIDHAA BORA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Judith Ferdinand, Mwanza
Wajasiriamali wadogo wa mkoniMwanza, wamepatiwa mafunzo na mbinu za kuweza kubuni bidhaa bora, zinazokubalika katika soko la ndani na nje sambamba na kuokoa muda, ili kuinua uchumi binafsi na taifa.
Hayo yalibainishwa jana na Mkurugenzi wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) tawi la Mwanza Mwl.Gordian Bwemelo, ambaye ni mgeni rasmi katika semina ya kuwajengea uwezo wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora na zenye tija kupitia mradi wa Kaizen wa nchini Japan ulio chini ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, iliofanyika mkoani hapa.
Bwemelo alisema,ili kukabiliana na ushindani wa soko,lazima kubadilika na kuacha kufanya vitu kwa mazoea kwa kubuni njia za kuzalisha bidhaa bora, hivyo Kaizen inakuja na mafunzo rahisi yatakayo wasaidia wajasiriamali.
Pia alisema, dunia imebadilika watu wanataka matendo siyo maneno, hivyo amewaomba washiriki wa semina hiyo kuyafanyia kazi yale waliyofundishwa na kuelekezwa, ili yaweze kuleta tija katika ushindani wa soko kwa kuzalisha bidhaa bora.
Hata hivyo alisema, wajasiriamali watumie semina na mafunzo mbalimbali kujifunza, kwani baada ya vita ya pili ya dunia nchi ya Japan ilibaki bila kitu, ila sasa ipo juu kiuchumi kutokana kuwekeza katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wananchi kutumia maliasiri.
Naye Kiongozi wa Mradi wa Kaizen Takao Kikuchi alisema,mradi huo ni baina ya nchi mbili Japan na Tanzania kwa ajili ya uendelezaji wa bidhaa zenye tija katika mazingira salama na kuokoa muda.
Pia alisema, Kaizen itasaidia kukuza uchumi wa nchi kwa kupitia viwanda itakavyotoa ajira kwa wananchi.
Kwa upande wake Ofisa Biashara Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Julieth Lema alisema, kupitia mafunzo hayo, yatawasaidia wajasiriamali kuzalisha bidhaa bora katika mazingira salama na kuokoa muda ili kuendana na soko la ushindani.

No comments: