LIVE STREAM ADS

Header Ads

MISA-TAN yafanya uzinduzi wa chapisho la upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
dsc_0550
Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) imetoa tuzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliyopewa jina la UFUNGUO WA DHAHABU kwa kuwa taasisi inayofunguka zaidi kwa wananchi hapa Tanzania kwa mwaka 2016. 

Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika jana katika hoteli yaa Sea Shells, Jijini Dar es Salaam.

Katika tuzo hizo Wizara ya Sheria na Katiba imeambulia Kufuli la Dhahabu kwa kuwa taasisi ngumu kwa upatikanaji wa taarifa kwa Umma.

MISA Tanzania pia walizindua Ripoti ya kila mwaka ya Upatikanaji Taarifa katika Taasisi za Umma kwa mwaka 2016.
Na Rabi Hume
Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumzia vigezo vilivyotumika kuchagua taasisi zilizofanyiwa utafiti mwaka huu, Utafiti uliofanywa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) katika katika Siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa ambayo huadhimishwa kila mwaka Septemba 28.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania,Bw. Roeland Van De Geer akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa (hawapo pichani) kwenye siku ya Kimataifa ya Haki ya Kupata Taarifa zinazoadhmishwa Septemba 28 kwa kila mwaka. Hapa ni ukumbi wa Hoteli ya Sea Shells iliyopo jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Chapisho la upatikanaji taarifa kwenye taasisi za umma. 
Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Bw. Roeland Van De Geer( wa pili kutoka kulia) na Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa( wa pili kutoka kushoto) pamoja na wadau mbalimbali wakiwaonesha waandishi wa habari pamoja na wageni waalikwa Chapisho la Upatikanaji Taarifa kwa taasisi za umma.
Baadhi ya viongozi wa Klabu za waandishi wa habari nchini pamoja na wadau mbalimbali wa habari wakiendelea kufuatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidi.

No comments:

Powered by Blogger.