VIKUNDI VYA UJASIRIAMALI KATIKA MANISPAA YA ILEMELA MKOANI MWANZA VYANUFAIKA NA FEDHA ZA MFUKO WAJIMBO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Judith Ferdinand, Mwanza
Vikundi 20 vya ujasiriamali vya wanawake na vijana katika halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani mkoani Mwanza, vimenufaika na fedha za mfuko wa jimbo lengo likiwa ni kuvisaidia kujikwamua kiuchumi kupitia miradi yao.
Meya wa Manispaa hiyo, Renatus Mulunga, amewakabidhi hundi ya shilingi milioni 40 kwa vikundi hivyo ambapo kila kimoja kitapata milioni mbili.
Mulunga alisema, vijana na wanawake wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii na kutumia fedha hizo vizuri, ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili katika biashara na miradi yao.
“Tumewapa mkopo wa milioni 40 mtarejesha kwa miezi kumi na mbili kwa asilimia 10 ya mkopo wenu, kwa ajili ya kuendeleza miradi yenu, hivyo tutawafatilia na kuhakikisha mnarejesha kwa wakati ili na vikundi vingine viweze kukopa, kwani manispaa hii kuna vikundi zaidi ya 1000, katika kata zetu tunataka kila kikundi kulichosajiliwa kipate fedha hizi na kuweza kujikwamua kiuchumi,”alisema Mulunga.
Alisema watu wanatakiwa kuwa na juhudi ya kufanya kazi kwa bidii pamoja na kujiunga katika vikundi kwani Serikali haiwezi kugawa fedha kwa kila mtu,ambaye hajishughulishi.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii, Afya na Elimu, Sarah Nghwani, alisema, fedha hizo zitatolewa kwa wanawake asilimia tano na vijana tano ili wawaeze kufanya kazi kwa pamoja na kurejesha fedha hizo kwa wakati.
“Nawaomba fedha hizi mkazitumie vizuri kwani siyo za luzuku tumewakopesha, mkazifanyie biashara,sambamba na kurejesha kwa wakati ili na wenzenu waweze kukopa , pia mkawe mabalozi kwa vikundi vingine ambavyo havijasijiliwa viweze kujisajili na kupata mkopo kwani kuna watu wa naogopa kukopa.
No comments: