LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKALI WA SASA BASI KUTOKA JIJINI MWANZA, LAU WA JOHN AZIDI KUKAA MIOYONI MWAO.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Alizaliwa June 18 miaka kadhaa iliyopita na wazazi wake wakampatia jina la Laurent John. Haikupita miaka mingi, akatambua kipaji chake cha uimbaji wenye kukonga na kugusa nyoyo za wanaoujua vyema muziki na akaanza kukitumia. Lau Wa John likawa jina lake kwenye muziki.

"Nakumbuka nilianza kumfahamu Lau wa John kupitia wimbo wake wa Kinara kupitia kwenye redio za Mwanza. Nikajikuta naanza kufuatilia nyimbo zake na hadi sasa mimi ni shabiki wake mkubwa hapa Mwanza". Anasema Janeth, mmoja wa mashabiki wa Lau Wa John akiwa mtaa wa Makoroboi Jijini Mwanza.

Janeth ambaye ana biashara zake za nguo Makoroboi, anasema nyimbo za Lau Wa John ikiwemo "Kinara" pamoja na wimbo mpya uitwao "Sasa Basi", zimekaa moyoni mwake na hujikuta tu akiziimba muda wowote.

"Asikwambie mtu jamaa anaimba. Kila siku lazima nisikilize huu wimbo wake mpya uitwao Sasa Basi. Akiendelea na mwendo huu, Mwanza itakuwa imeongeza kichwa kingine kwenye muziki". Anadokeza Mwana Kwetu, mkurugenzi wa kampuni inayouza vifaa vya ulinzi Mtaa wa Uhuru Jijini Mwanza.
Bonyeza HAPA Kusikiliza na Kupakua Sasa Basi au Bonyeza Play Hapa Chini.

No comments:

Powered by Blogger.