LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAANA HALISI KUHUSU SIKUKUU YA EID EL HAJJ.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Idd El Hajj ni sikukuu ya Uislamu wakati wa mwezi wa Dhul Hijjah ambao ni mwezi wa Hajj. Husheherekewa kama kumbukumbu ya sadaka ya Ibrahimu (Abrahamu) ambaye kufuatana na taarifa za Biblia na za Qurani alikuwa tayari ya kumchinja mwanawe kama sadaka kwa Mungu.

 Lakini Mungu alimzuia asimchinje akampatia kondoo badala yake. Habari zake kati Qurani ziko sura al-Hajj aya 37, katika Biblia Mwanzo 22.

Kila Mwislamu mwenye uwezo hupaswa kumchinja mnyama wa sadaka siku hiyo mara nyingi kondoo lakini kuna pia sadaka za mbuzi, ng'ombe au ngamia kufuatana na uwezo na kawaida ya nchi.

Sehemu ya nyama ya sadaka hizo hugawiwa kwa maskini wasio na uwezo. Nyingine hutumiwa kwa karamu ya wafamilia.
BMG inawatakia Waislamu wote ndani na nje ya Tanzania, Sikukuu Njema ya Edd El Hajj. Eid Mubarak!
Kuhusu Picha Bonyeza HAPA

No comments:

Powered by Blogger.