SHIRIKA LA "NI HEKIMA PEKEE" LATAKA WATOTO WASIOJUA KUSOMA NA KUANDIKA KUSAIDIWA.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Na Judith Ndibalema, Mwanza
Jamii imetakiwa
kushirikiana na Serikali pamoja na wadau mbalimbali wa elimu ili kuwanusuru
watoto walio mitaani ambao hawajui kusoma wala kuandika Jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Shirika
lisilo la kiserikali la Ni Hekima Pekee, linalowahudumia watoto wanaoishi
katika mazingira hatarishi Jijini Mwanza, Onesmo Kajuna, ametoa rai hiyo wakati
akizungumzia hatari inayowakabiri watoto hao ikiwa watakosa fursa ya kupata
elimu.
Amesema ushirikiano wa
karibu miongoni mwa jamii, serikali pamoja na wadau wote wa elimu, utasaidia mpango
wa MEKWA unaolenga kuwafundisha watoto wenye umri mkubwa nchini kujua kusoma
na kuandika kufikia malengo yake.
Kajuna ameongeza kwamba
watoto wakipata elimu, watajiepusha na utumiaji wa dawa za kulevya, ndoa pamoja
na mimba za utotoni hivyo jamii inapaswa kuhakikisha hakuna mtoto anayekosa
fursa ya kwenda shule ikizingatiwa kwamba elimu ya msingi na sekondari nchini
inatolewa bure.
No comments: