LIVE STREAM ADS

Header Ads

TAASISI YA MIFUPA NA MISHIPA YA FAHAMU MOI YAPOKEA MSAADA WA MIGUU BANDIA KWA AJILI YA WAHITAJI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Displaying MOI 06.jpg
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu MOI, Dkt. Othman Kiloloma (kulia) akionesha moja ya viungo bandia wakati wa makabidhiano ya msaada wa miguu ya bandia takribani 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 60 kwa ajili ya kuwasaidia wagonjwa wenye mahitaji ya viungo hii leo.

Na James Salvatory BMG Dar
Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu, katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili Jijini Dar es salam (MOI), imepokea msaada wa miguu bandia ipatayo 600 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 60 kwa ajili ya kuwasaidia wahitaji.

Kaimu Mkurugezi wa MOI Dkt.Othamani Kiloloma, amesema miguu hiyo ni ya watu wazima na watoto ambapo inatarajiwa kutumika katika maabara ya kutengenezea viungo bandia ya MOI ili kuzalisha miguu mingine ambayo itasaidia watanzania ambao  wamepoteza viungo kutokana na sababu mbalimbali.

Aidha Kiloloma amesema msaada huo umetolewa na taasisi ya Legs 4 Africa ya Uingereza, kwa kushirikiana na asasi ya Mohamed Punjani ambazo zimekuwa zikitoa misaada mbalimbali kwa watoto, walemavu ,wazee na watu wenye mahitaji maalum hapa nchini.

No comments:

Powered by Blogger.