LIVE STREAM ADS

Header Ads

TFDA yavunja Stoo na kukamata Dawa Bandia mkoani Mara.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Ofisi ya Kanda ya Ziwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi imelazimika kuvunja Stoo ya kuhifadhi Dawa bandia katika mtaa wa Uhuru Mkendo katika Manispaa ya Musoma mkoani Mara.

Uamuzi wa kuvunja stoo hiyo iliyodaiwa kumilikiwa na mfanya biashara wa Dawa za binadamu, Juma Maswe Nyamgambwa, ulifanywa baada ya aliyetajwa kuwa mmiliki kuwaambia maafisa wa TFDA kwa njia ya simu kuwa haifahamu stoo hiyo.

Mkaguzi wa Dawa wa TFDA, Venance Burushi, alisema kuwa walipewa taarifa na msiri kuwa stoo hiyo ilikuwa ikihifadhi dawa na kuamua kufanya ukaguzi katika chumba hicho kilichoko katika nyumba namba Na. 39 inayomilikiwa na Bi Zubeda Yusufu. 

“Tulimwambia Juma Maswe Nyamgambwa tuliyeambiwa kuwa mmilikiki wa chumba hicho atulete eneo hili ili tufanye ukaguzi lakini akatueleza kuwa hausiki na stoo hiyo. Tuliamua kuvunja chumba hicho ili tuweze kufanya ukaguzi kwa mujibu wa sheria ya Chakula na Dawa sura Namba 219” alisema.
Burushi anaeleza kuwa baada ya kufungua ghala hilo walibaini uwepo wa dawa nyingi huku baadhi zikiwa hazina usajili zenye thamani inayokadiriwa kuwa TZS 4,384,000/-. “Tulibaini pia uwepo wa dawa zinazosadikika kuwa bandia aina ya praziquantel (makopo 209) na quinine ya kiwanda cha Keko Pharmaceuticals Industry (makopo 15) zote zikiwa na thamani ya TZS 4,512,000/- , dawa za serikali ya Tanzania aina ya Depo provera (chupa 1775) zinazokadiriwa kuwa na thamani ya TZS 1, 775,000/-, dawa za serikali ya Uganda zenye thamani ya TZS 245,000/- pamoja na dawa zenye usajili pamoja na vifaa tiba vinavyoashiria kuingizwa nchini kinyume na Sheria vyenye thamani ya TZS 8,295,000/-. Jumla ya dawa na vifaa tiba vilivyokamatwa katika ghala hilo vilikuwa na thamani ya TZS 19,211,000/-’’ alisema.

Aidha Burushi alisema kuwa ingawa ndani ya chumba hicho walikuta dawa ambazo sio bandia lakini chumba hicho hakifai kwa kutunza dawa. “Chumba kilikuwa na vitu vingine vingi kama vile vifaa vya magari. Mazingira tuliyakuta kwenye chumba hayafahi kuhifadhi dawa na neneo hili halijasajiliwa na TFDA kwa ajili ya kuhifadhi dawa” alisema.

Zoezi hilo lililovuta hisia za wakazi wengi wa Manispaa ya Musoma  ilishuhudiwa na Viongozi wa Wilaya na Manispaa ya Musoma akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Vicent Anney Naano, Mkurugenzi wa Mnispaa ya Musoma Fidelica Myovella, Mganga Mkuu wa Manispaa Dkt. Honoratha Rutatinisibwa na Kaimu Mfamasia wa Manispaa Less Sumni.
Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya Musoma Dkt. Vicent Anney Naano alisema kuwa aliamuru kuvunjwa kwa chumba hicho ili kukamata dawa hizo katika harakati za kukomesha bidhaa bandia katika Manispaa ya Musoma na mkoa kwa ujumla. “ katika ukaguzi wa awali TFDA walibaini uwepo wa dawa za bandia za kichocho katika maduka mengi binasfi ya kuuza dawa. Hali hii ilitushitua sana. Kwa hiyo tulivyopata taarifa za msiri niliagizi jeshi la polisi kuvunja chumba hicho kwa kushirikiana na TFDA”.

Dkt. Naano aliongeza kuwa walifuata taratibu kwa kuwaita viongozi wa mtaa, mtendaji wa kata na diwani tukavunja. “Wakaguzi wakafanya ukaguzi. Tulichokikuta huko ndani kinasikitisha. Kulikuwa na maboksi ya bidhaa bandia ambazo zimewekwa katika vifungashio vya makopo ya mafuta ya kupaka” a;isema.

Mmiliki wa nyumba hiyo Bi. Zubeda Yusufu alidai kuwa licha ya Juma kukataa kumiliki duka hilo lakini yeye ndiye aliyempangisha. “Anakitumia chumba hiki karibu mwaka wa tatu sasa. Majirani wote wanajua. Nimeongia nae mkataba ambao uko kwa ndugu zangu Dar es Salaam” alisema.

No comments:

Powered by Blogger.