WAKAZI WA WILAYA YA IKUNGI MKOANI SINGIDA WAMPONGEZA MKUU WA WILAYA HIYO.
Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com
Wananchi wa Mji wa Ikungi Mkoa wa Singida, wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu, kwa kuwaelimisha juu ya kushirikiana na serikali ikiwemo uchangiaji wa hiali wa miradi ya maendeleo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi mjini humo.
“Mkuu wa Wilaya tunakupongeza kwa uamuzi wako wa kufanya mikutano ya hadhara ya kuwaelimisha wananchi pamoja na kusikiliza kero mbalimbali ambazo zimeshindwa kupatiwa majibu na kutafutiwa ufumbuzi kwa muda mrefu, kwa utaratibu huu sasa DC Mtaturu umefungua milango ya wananchi kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu,”alisema Juma Seleman.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mtaturu akihutubia mamia ya wananchi ikiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu kuteuliwa na Rais Dk John Magufuli kushika wadhifa huo, alisema kwamba wananchi wa maeneo yote ya Wilaya ya Ikungi wanao wajibu wa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani katika kuchangia shughuli na miradi ya maendeleo itakayowezesha upatikanaji bora wa huduma za kijamii.
Mtaturu alisisitiza kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyo chini ya uenyekiti wake haitawavumilia wale wote watakaopita katika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata kuwazuia wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo uchangiaji wa hiali, pia kupandikiza chuki na kufanya uchochezi kwa lengo la kuvuruga amani na kureta machafuko, watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
"Wito wangu kwa watendaji wa serikali ni kuwatumikia wananchi na kuachana na utendaji wa mazoea wa kujifanya miungu watu hasa kwa watendaji wa vitongoji, vijiji na kata na badala yake tujikite kutatua kero na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka, huku akiwataka wataalamu wa Halmashauri katika sekta za mifugo, kilimo, afya, elimu na uchumi kuwatumikia wananchi kwa weredi kama serikali inavyoahidi". Aliongeza Mtaturu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu, akihutubia wananchi wa mji wa Ikungi katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali na kutolea ufafanuzi hoja za wananchi huku akiwahamasisha na kuwaelimisha kushirikiana na serikali iliyopo madarakani kushiriki shughuli za maendeleo na kudumisha amani.
Na Peter Fabian, Singida
Wananchi wa Mji wa Ikungi Mkoa wa Singida, wamempongeza Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Miraji Mtaturu, kwa kuwaelimisha juu ya kushirikiana na serikali ikiwemo uchangiaji wa hiali wa miradi ya maendeleo katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi mjini humo.
“Mkuu wa Wilaya tunakupongeza kwa uamuzi wako wa kufanya mikutano ya hadhara ya kuwaelimisha wananchi pamoja na kusikiliza kero mbalimbali ambazo zimeshindwa kupatiwa majibu na kutafutiwa ufumbuzi kwa muda mrefu, kwa utaratibu huu sasa DC Mtaturu umefungua milango ya wananchi kushirikiana na serikali katika shughuli za maendeleo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya yetu,”alisema Juma Seleman.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Mtaturu akihutubia mamia ya wananchi ikiwa ni mkutano wake wa kwanza tangu kuteuliwa na Rais Dk John Magufuli kushika wadhifa huo, alisema kwamba wananchi wa maeneo yote ya Wilaya ya Ikungi wanao wajibu wa kushirikiana na serikali iliyopo madarakani katika kuchangia shughuli na miradi ya maendeleo itakayowezesha upatikanaji bora wa huduma za kijamii.
Mtaturu alisisitiza kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama iliyo chini ya uenyekiti wake haitawavumilia wale wote watakaopita katika maeneo ya vitongoji, vijiji na kata kuwazuia wananchi kushiriki shughuli za maendeleo ikiwemo uchangiaji wa hiali, pia kupandikiza chuki na kufanya uchochezi kwa lengo la kuvuruga amani na kureta machafuko, watachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
"Wito wangu kwa watendaji wa serikali ni kuwatumikia wananchi na kuachana na utendaji wa mazoea wa kujifanya miungu watu hasa kwa watendaji wa vitongoji, vijiji na kata na badala yake tujikite kutatua kero na kuzitafutia ufumbuzi wa haraka, huku akiwataka wataalamu wa Halmashauri katika sekta za mifugo, kilimo, afya, elimu na uchumi kuwatumikia wananchi kwa weredi kama serikali inavyoahidi". Aliongeza Mtaturu.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi mkoani Singida, Miraji Mtaturu (kulia), akimsikiliza Mkuu wa Polisi Wilayani humo (OCD), Milton Nkyalu (kushoto), wakati akitoa majibu na ufafanuzi wa hoja za wananchi. OCD Nkyalu aliwataka kutoa taarifa za siri za watu wanaojihusisha na kutekeleza matukio ya uhalifu na wizi wa mifugo katika maeneo mbalimbali ya Wilaya hiyo.
No comments: