LIVE STREAM ADS

Header Ads

WAZIRI LUKUVI AFUTA HATI ZA VIWANJA VYA WAZI VILIVYOMILIKISHWA KIMAKOSA JIJINI DAR ES SALAAM.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory, BMG Dar
Waziri wa  ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi, Williamu Lukuvi, amefuta usajili viwanja namba 213, 215 na 217 block b kinyerezi Jijini Dar es salaam, ambavyo vilimilikishwa kimakosa kwa wananchi kwani viko katika eneo la wazi kwa ajili ya makaburi.

Alisema eneo ambalo wananchi wamekuwa wakilitumia kwa ajili ya makaburi kwa muda mrefu limekutwa limepimwa viwanja vitatu kwa ajili ya matumizi mengine  ambapo amewataka wamiliki wa viwanja hivyo kufika ofisini kwake kueleza namna walivyopata umiliki wa viwanja hivyo.

Lukuvi ameagiza wote waliohusika na utoaji wa namba na hati kwenye mchoro wa viwanja hivyo kuchukuliwa hatua za kisheria.

1 comment:

  1. Hapo hapo Kinyerezi kuna figisufigisu nyingi wajane wanadhulumiwa haki zao kwa kunyang'anywa nyumba. Mwenyekiti wa serikali za mitaa yupo na anajua kila kitu lakini wananyamazia. Hakimu wa mahakama ya Buguruni anajua lakini naye anajua alichokifanya. Ombi: Tafadhali sana viongozi wote wanaojua tatizo la Bibi Jabiri la kutolewa nje ya nyumba ya wanawe mapacha waliokufa kwa ajali ya gari na kisha kudhulumiwa kwa kunyang'anywa nyumba yao tena kwa masimango na vitisho wamsaidie mama huyo kupewa haki yake kisheria. Naamini Mungu amewapa watu uongozi ili waweze ktenda mema kwa kuwasaidia watu wanaowaongoza na makundi maaluum kama wajane, waathirika, wagonjwa na binadamu wengine ambao hawakupewa tunu hiyo ya kuongoza jamii. Fedha zitatupeleka wapi? Maisha yetu kama maandiko yanavyodhihirisha ni mafupi mno chuini ya jua hili. Ni kwanini tusiwaonee binadamu wenzetu huruma? Kwa nii tumekuwa na mioyo migumu hadi kufikia kudhulumu nyumba za wajane kwa deni alilokopa marehemu la Tsh. 1,700,000/= tu? Ni kiwanja gani Dar hii kinauzwa kwa bei hiyo? Je, huyo hakimu aliyeamuru nyumba ichukuliwe kwa deni la bei hiyo alikuwa na akili timamu wakati anatoa hukumu hiyo? Na, Je, Mdai wakati wa mazishi ya marehemu alikuwa wapi asitamke kuwa anadai familia hiyo kiasi hicho cha fedha? Naomba viongozi wote wanaojua kutenda haki waingilie kati suala hili.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.