LIVE STREAM ADS

Header Ads

KESI YA KUPINGA MATOKEA JIMBO LA BUNDA MJINI YAANZA KUSIKILIZWA MKOANI MARA.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na Rose Jacob na Rose Joseph,Musoma-Mara
Mahakama kuu inayoketi katika Wilaya ya Musoma mkoani Mara, imehairisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 katika jimbo la Bunda mjini ambayo imendelea kuunguruma takrani miezi 11 tangu kuanza.

Kesi hiyo ambayo itaanza kusikilizwa oktoba 5 mwaka huu katika Mahakama hiyo, Jaji Noel Chocha, alipokea Shauri hilo jana na kupitia hoja  muhimu na zile ambaZo aliona hazina umuhimu walikubaliana kwa pamoja na mawakili wa pande zote mbili kuziondoa ili kufanyia kazi hoja zitakazo bishaniwa.

Jaji Chocha aliainisha hoja zitakazobishaniwa katika kesi hiyo kuwa ni hitilafu zinazo lalamikiwa zilijitokeza wakati wa uchaguzi, mfano kama vituo vilivyoongezeka wakati wa kuhesabu kura,utofauti wa hidadi ya vituo vya kupigia kura Bunda mjini, ikiwa na msimamizi wa kituo cha kuhesabia kura wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) alilalamikia  kuwepo kwa tuhuma za kampeni haramu na hakuna hatua ambazo zilichukuliwa.

Baada ya jaji kupokea shauri hilo ndipo mawakili wapande zote mbili waliomba waliomba Makahama hiyo iwapatie masaa 48 ili wapate muda mzuri wa kukaa na kutafakari ili kujiweka sawa pidi kesi itapo anza.
Bonyeza HAPA Kujua Zaidia

No comments:

Powered by Blogger.