LIVE STREAM ADS

Header Ads

KESI YA KUPINGA MATOKEO JIMBO LA BUNDA MJINI, WASIRA ARINDIMA MAHAKAMANI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com


Na Rose Jacob, Musoma
SHAHIDI wa tatu katika kesi namba moja ya mwaka 2015 ya kupinga matokeo yauchaguzi katika jimbo la Bunda mjini, Steveni Wasira, jana alichukua muda wa saa tano kutoa utetezi wake huku akidai uchaguzi huo haukuwa huru na haki kutokana na kugubikwa na ongezeko la idadi ya wapiga kura kutoka 69,369 iliyokuwa imetolewa na msimamizi wa uchaguzi kwa vyama vilivyo shiriki.

Wasira alisema wakati wa kutangaza kura za mshindi, msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo L.Msofe alitangaza kura 164,794 wakati ilikuwa ni kinyume cha idadi ya hapo awali aliyokuwa ameisha itoa.

Shahidi huyo aliimbia Mahakama hiyo alimwandikia barua msimamizi wa uchaguzi katika jimbo hilo ili kutaka kurudia kuhesabu kura, kutokana hakupata barua inayoonyesha niwapi na nimuda gani watakapo anaza kuhesabu kura hizo, lakini msimamizi huyo alifanya kinyemela jambo ambalo hakukubaliana nalo.

Vile vile alidai kufanyika kwa kampeni zilizofanywa na baadhi ya
 Wasimamizi wa vituo na baadhi ya wafuasi wa walalamikiwa hivyo alipata taarifa kutoka kwa Samweli Makindi aliyekuwa wakala wa kituo cha Nyamatoke shule ya Msingi namba mbili na kufika na kujione hali iliyokuwepo ikiendelea na alithibitisha yeye mwenyewe kitendo hicho.

Naye wakili wa wajibu maombi Tundu Lisu aliomba Makamai hiyo kuondoa baadhi ya Aya ya 3’ B’katika kiapo caha shahidi Steven Wasira aliyekuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, kutokana na kuleta sura mpya ambayo haipo katika hati ya maombi yakesi hiyo. 

Aidha  Jaji wa Mahakama hiyo Noel Chocha, alikubaliana naombi la wakili Tundu lisu lakutaka kuondoa baadhi ya vifungu ambavyo ni aya ya 3’B’ Mstali wapili hadi wane vilivyo kuwa vikitaja majina ya vituo vilivyoongezwa na msimamizi wa uchaguzi katika baadhi ya maeneo,baada ya wakili wa upande wa waleta Maombi Costantin Mtalemwa  kulizia viondolewe maana hata  kama vitaondolewa havita athiri kesi hiyo.

Aidha wasira aliielezea mahakama kuwa  alitambua kuwa baadhi  vituo viliongezekaVituo tisa na kuwa 199 badala ya 190.
Vituo alivyoweza kuvitambua vimeongezeka alivitaja kuwa ni pamoja na kata ya Kabasa ambapo kiliongezeka kitui kimoja,stoo Nyasana,Bunda mjini kilichongezeka ofisi ya VEO,Bunda stoo,ofisi ya halmashauri jengo la kilimo,katika kijiji cha Manyamanyama kata ya Nyamakokoto viliongezeka vituo vituo vitatu ambavyo ni  Bunda DDH,Balili'A' shule ya Msingi na Balili 'B' shule ya Msingi.

Vituo vingine ni  kata ya Wariku kituo shule ya msingi Kamkenga,kata ya Guta shule ya msingi Nyantare na kituo cha Benki kata.

Katika vituo tisa vilivyoongozeka Wasira anavyolalamikia alisema CCM hawakuwa na mawakala  kutokana na kutokuwa na uhalali hali ambayo  CCM hawakuweka mawakala kwani vituo hivyo vilikuwa si halali kisheria na kwamba asingeweza kutambua idadi ya waliopiga kura katika vituo hivyo.

No comments:

Powered by Blogger.