LIVE STREAM ADS

Header Ads

MAUZO YA HISA YAPANDA SOKO KUU LA HISA DAR ES SALAAM DSE.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Na James Salvatory BMG Dar
Hali ya nguvu ya soko katika soko la hisa la Dar es salaam (DSE) katika kaunta ya kampuni ya sigara nchini imeelezwa kuwa chanzo kikuu cha kupanda kwa mauzo ya hisa katika soko la Dar es salam.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam Afisa mwandamizi wa soko hilo Mary Kinabo, alisema hali hiyo imechangia mauzo ya hisa kuongezeka kwa asilimia 65 kutoka
shilingi bilioni 19.6 hadi kufikia shilingi bilioni 32.2 kwa wikihii .

Alisema wakati takwimu zinaonesha idadi ya hisa zilizouzwa na kununuliwa imepanda zaidi ya mara nne kutoka hisa milioni 2.4 hadi kufikia hisa milioni 9 wakati huo huo makampuni
yanayoongoza nipamoja na CRDB (70%) ikifuatiwa kampuni yasigara ya TTC(25%) huku hisa za TBL zikiuzwa kwa asilimia 3.

“Wakati benki ya CRDB ikiongoza kuuza hisa zake kwa asilimia sabini ukubwa wa mtaji wasoko umeshuka kwa asilimia 0.41 kutoka trilioni 21.576 hadi kufikia shilingi trioni 21.49 hali iliyochangiwa na kushuka kwa kaunta za NMG pamoja nakampuni ya ACA.

“Ukubwa wamakampuni ya ndani umepanda kwa asilimia0.35 kutoka trilioni 8.1 hadi trioni8.13 hali iliyochangiwa nakushuka kwa bei katika kaunta ya TBL;

''Sekta yaviwanda imepanda kwapointi 26.16 baada ya hisa za TBL kupanda kwa asilimia 0.77 ikilinganishwa na kushuka kwa sekta
yahuduma yakibenki kushuka 0.52 baada ya bei kushuka kwenye kaunta yaDSE kwa asimilia 1.54" Alisema kinabo.

No comments:

Powered by Blogger.