LIVE STREAM ADS

Header Ads

HALMASHAURI NCHINI ZATAKIWA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUKUZA NA KUENDELEZA BIDHAA ZA NGOZI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for BIDHAA ZA NGOZIJudith Ferdinand, Mwanza
Halmashauri  zote nchini  pamoja na wananchi kwa ujumla, zimetakiwa kuunga mkono  juhudi za Mamlaka ya Kuendeleza Biashara Tanzania (TAN TRADE), za kukuza, kuendeleza na kutangaza bidhaa za ngozi,ili kukuza uchumi binafsi na taifa.

Wito huo ulitolewa jana na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAN TRADE Edwin Rutageruka, wakati akizungumza na majira kwa njia ya simu.

Rutageruka alisema, ili kuendeleza bidhaa za ngozi zinazozalishwa nchini, halmashauri inatakiwa kuunga mkono juhudi za mamlaka hiyo kwa kuelekeza  wazazi kununua viatu vya shule vya watoto
vinavyotengenezwa    na wajasiriamali wa ndani.

Pia alisema,wananchi wanatakiwa kununua bidhaa za ngozi zinazozalishwa ndani ya nchi, ili kukuza,kuendeleza sekta hiyo sambamba na kuongeza ajira,uchumi binafsi na taifa kwa ujumla.

Hata hivyo alisema, mpaka sasa wajasiriamali wanauwezo wa kuzalisha bidhaa za ngozi nyingi na zenye ubora,kutokana na kuunda umoja wao wenye wanachama 150 unaoitwa Umoja wa Wazalishaji wa Bidhaa za Ngozi Tanzania ( TALEPPA).

Vilevile alisema, wajasiriamali hao mpaka sasa wanaweza kuzalisha bidhaa za ngozi mbalimbali ikiwemo viatu vya watoto wa shule za msingi na sekondari, mipira pamoja na viatu vya askari jeshi, zinazokidhi soko  la  ndani na nje.

Aidha alisema mamlaka hiyo, kupitia mkutano mkuu wa mwaka wa Jumuiya za  Mamlaka ya Serikali za Mitaa Tanzania(ALAT), uliofanyika   mwezi semptemba mwaka wilayani Musoma mkoani Mara   ilipata fursa ya kuhimiza viongozi wa halmashauri zote nchini, kuhamasisha wananchi kununua bidhaa za ngozi zinazozalishwa  na wajasiriamali wa ndani.

Kadhalika alisema, mamlaka hiyo itaendelea na  juhudi za kukuza na kuendeleza bidhaa za ngozi, za ngozi sambamba na kuhimiza jamii kupenda bidhaa hizo,ili kuongeza ajira na uchumi binafsi na taifa.

No comments:

Powered by Blogger.