LIVE STREAM ADS

Header Ads

MKIMBIZA MWENGE KITAIFA ATOA MAAGIZA KWA HALMASHAURI NCHINI.

Ikiwa Una Habari, Tukio, Picha, Maoni au Tangazo, Wasiliana Na BMG Kwa Nambari za Simu 0757 432694 Au Email binagimediagroup@gmail.com

Image result for MWENGE
Na Shaban Njia, Kahama
Halmashauri nchini zimetakiwa kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya ujasiriamali kwa vijana sambamba na kutochelewesha asilimia tano ya mikopo zinazostahili kwenda kwa vijana.

Agizo hilo lilitolewa na Mkimbiza Mwenge Kitaifa, Alex  Kayuni, wakati akitoa ujumbe wa Mwenge kwa wakazi wa Kata ya Isaka,kwa kuhimiza Halmashauri juu ya utengaji wa maeneo hayo kwa lengo la kuongeza vipato kwa vijana,kukuza maendeleo ya eneo husika na uchumi wa nchi.

Aidha aliikumbusha  halmashauri ya Msalala mkoani Shinyanga kuhakikisha inaanzisha SACCOS ya vijana itakayohusika na kutoa mikopo  kwa vijana huku akisisitiza kuwa asilimia tano ya mapato yake ya ndani katika kila halmashauri,zinawafikia kwa wakati vijana kusudi wafanye shughuli za ujasiriamali zenye tija na kujenga uchumi wa nchi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo hilo, Ezekeil Maige, aliomba Serikali ya awamu ya tano kuwaunga mkono katika juhudi zao za kuleta maendeleo katika Halmashauri hiyo,kwa kuhakikisha inawapatia kwa wakati pesa zilizopangwa katika bajeti kwa ajili ya miradi.

Nae Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu,alisema mbio za Mwenge katika Halmashauri hiyo zimetumia kilometa 216,kwa kupita katika tarafa mbili,kata saba na kupitia miradi kumi ya maendeleo iliyoibuliwa na wananchi, serikali pamoja na tasisis binafisi ambapo baadhi ilikaguliwa,kuzinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi,ambapo miradi yote hiyo ghaalimu jumla ya Shilingi Bilioni  2.386/=.

No comments:

Powered by Blogger.